Dawa hii ni katika madawa makubwa sana ambayo yalikuwa yanatumika tangu enzi za mitume rehema na amani ziwe juu yao
leo ntawajuza baadhi ya faida za habbatsauda ya chenga
baadhi ya magonjwa yanayotibiwa na habbatsauda ni
Hutoa minyoo ya aina zote
huponyesha maradhi ya mabaranga
hutibu homa za vipindi
husafisha malendalenda machafu yanayokuwa kooni na kifuani
huzibua mishipa iliyoziba kwa uchafu au ugonjwa wowote
huondoa gesi tumboni
hukausha unyevunyevu ulio kwenye fuko la chakula kwani fuko la chakula kitaalam halitakiwi kupata unyevunyevu
husaga na kuyeyusha vijiwe vilivyopo kwenye mafigo na kibofu cha mkojo
huteremsha hedhi ambazo zimejifunga kabla ya wakati
hufungua njia ya mkojo na mtu akapata mkojo vizuuuri
hukusanya maziwa na kufanya yatoke mengi kwa mwanamke aliyejifungua kisha maziwa yakawa machache
huponyesha mafua yanayosababishwa na baridi
NAMNA YA KUTUMIA HABBATSAUDA KUJITIBU MOJA KATI YA MARADHI HAYO HAPO JUU KAMA UNAYO
Tumia kijiko kimoja cha chai cha unga wa habbat sauda ndani ya glass1 ya maziwa fresh au chai ya moto au maji ya moto
kunywa kutwa mara3....kwa mwezi mmoja mpaka miezi 6 na utaratibu huu husaidia kutibu maradhi mengi mwilini,kwani kama mtu ataamua kutumia habbatsauda kwa kipimo hicho na ndani ya muda huo nilioutaja,mtu huyo anakuwa na uwezo wa kuzalisha askari wengi mwilini mwake ambao watakuwa wakipambana na maradhi mbalimbali...................
pia ni vizuri habbatsauda ifanywe kama chakula na iliwe wakati wowote hasa baada ya kila mlo 1x3 kwa kipimo nilichokitaja,jambo la msingi sana ni kutumia dawa hii kwa muda unaotosheleza
KUJITIBU VIJIWE KATIKA KIBOFU NA FIGO
Kwa ugonjwa huu chukua unga wa habbatsauda vijiko10 vya chakula kisha changanya na vijiko20 vikubwa vya asali,
matumizi
chota kijiko kikubwa cha mchanganyiko huo koroga ndani ya glass ya maji ya moto,kunywa siku mara3 kwa siku 21......
chota kijiko kikubwa cha mchanganyiko huo koroga ndani ya glass ya maji ya moto,kunywa siku mara3 kwa siku 21......
KUJITIBU MAFUA
mtu mwenye matatizo hayo achukue unga wa habbatsauda autie kwenye kitambaa awe ananusa kila baada ya muda atapona
hii ni mbegu ya habbatsauda ambayo husagwa na kupatikana unga wake au hukamuliwa na kupatikana mafuta ya habbatsauda,mafuta haya yanatibu maradhi mengi pia ntaelezea kwenye mada nyingne