Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumamosi, 24 Oktoba 2015

HUYU NDIYE JINNI GHUUL AU CHUMA ULETE



JINNI GHUUL A.K.A CHUMA ULETE)
Hawa ni majini wanaoshirikiana na wachawi katika kufanya mikataba ya kumtumikia mchawi kwa kumletea vitu vya wizi na mchawi huyo kumlipa jini damu,najisi nk

~Wachawi wakitaka kumtengeneza chuma ulete wanachukua vitu 9 ambavyo mjumuiko wake huitwa `KABBUN`

Kwanza wanachukua kidaka cha nazi,kinawekwa ktk chungu ambacho kinakuwa na mjumuiko wa vitu vingine  8 ikiwemo moja ni katika ngozi ya mjusi,

 baada ya kuichukua hii ngozi ya mjusi pia huichanganya kwenye vile vitu vya kwenye chungu,kisha vinapelekwa makaburini na kufukiwa huko na kukaa kwa siku 21~27 inategemea ni chuma ulete mwenye nguvu na uwezo kiasi gani anayeandaliwa.

~baada ya kutimu hizo siku mchawi yule anarudi kule makaburini na kukichukua kile chungu na anakuja navyo mpk sehemu maalum ambayo ameshaiandaa kwa kazi yake hyo ambapo ni lazima awe katandika kitambaa chekundu,cheupe au cheusi yategemea na ukubwa wa chuma ulete anayeandaliwa....

ataanza kusema maneno fulani ya kichawi kukiambia kile chungu na mara ghafla utaanza kuskika mvumo wa sauti mfano wa kundi kubwa la nyuki au upepo mkali na baada ya hapo unatoka moshi mkubwa ndani ya chombo kile na ataanza kuonekana mnyama mfano wa paka kisha ghafla atabadilika kuwa mtoto au mtu mzee sana....

hapo sasa yule mchawi wanaanza kuwekeana mikataba ya kutumikiana na yule jini...mikataba hyo mara nyingi huwa kila baada ya miaka,mwaka,miezi au hata mawiki awe yule jini anapewa damu ya mnyama,ndege au hata bin adam.......
 ~Basi hapo ndyo utaona watu wanapoteza maisha yao ktk mazingira ya ajabuajabu

baada ya makubaliano kufanyika hapo sasa ndyo mchawi anakuwa na uwezo wa kumuagiza popote jini huyu akamuibie mapesa ya watu,na ana uwezo wa kuiba pesa popote zilipo hata kama ni mfukoni mwako


Huyu jini anapofika kwenye nyumba ya mtu ni marufuku kuchukua hela zote lazma achukue robo au nusus tuu ya fedha aliyoikuta na kumpelekea mchawi wake....

Yule mchawi naye ni marufuku pesa hizo kufanyia maendeleo ya aina yyte tena kibaya zaidi anatakiwa asilale nayo bali aitumie na kuimaliza siku hyohyo ili kesho waanze hesabu mpya....
 pia jini huyu anapojigeuza jini mahaba mtu wake huwa na bahati sana ya kuokota pesa,kupewa pesa au kitu cha thanmani hata na mtu usiyemfahamu,pia binafsi nilishuhudia mama mmoja aliwahi kuletewa pesa nyingi mpk nyumbani kwake lakini baada ya kuanza kutibiwa pesa zile zilipotea kwenye mazingira ya ajabu.