Uadui kati ya majini na binadamu uliendelea sana na ukawa mkubwa kupita kiasi kutokana na wivu wa majini kutolewa kwenye utawala wa dunia kisha kuwekwa binadamu ndiye awe khalifa duniani.
uadui ulipozidi kushamiri majini wakaamua kumomba mwenyezi mungu mambo matatu
1.Waliomba mungu awape umri mrefu sana
2.Waliomba wapewe uwezo wa kujibadilisha kutoka hali moja mpaka nyingine
3.Sisi tusiweze kuwaona ila mpaka watake wenyewe
na katika maombi yao hayo kwa mwenyez mungu yote aliwapa na ikawa kama walivyoomba
Majini wanaishi miaka mingi sana kuliko hata sisi binadamu,ukisoma katika habari za maisha ya majini utakuta jini ambaye ni kijana mdogo ambaye kwa binadamu anakuwa ni mtu mwenye miaka kati ya 18 mpaka 25 kwa upande wa majini wao ni tofauti.
Jini ambaye ni kijana mdogo ni yule ambaye anakuwa amefika miaka 2500 hadi 3000 huyu ndiyo katika umri wa kibinadamu ni sawa na mwenye miaka 18 mpaka 25
Dua ya pili waliyoomba ni kubadilika nayo hii pia ilikubaliwa kwani majini wana uwezo wa kujibadilisha kutoka hali moja hadi nyingine.
Ameeleza mwanachuoni wa kiislam Shekh Ibn Taymiyya rehema ziwe juu yake katika kitabu cha Majmuui alfataawa anasema mtaalam huyo wa ulimwengu wa tiba za kisheria ''ALJINNU WA SSHAYAATWIINU AJSAAMUN'' akiwa na maana kuwa ''majini na mashetani wana viwiliwili''
sasa hapa utajiuliza ''inakuwaje jini anaingia ndani ya kiwiliwili cha watu na wanyama hali ya kuwa na yeye ana kiwiliwili??"
Ibn Taymiyya[r.a] anasema kuwa mwenyez mungu amewapa majini uwezo wa kujibadilisha wanavyotaka kutoka kwenye maumbile yao kwenda kwenye maumbile mengine
majini wana uwezo wa kujigeuza sura na umbo la mtu yeyote,kitu chochote na pia wana uwezo wa kujibadilisha hata upepo na hali hii ndiyo inayowawezesha kuingia katika miili ya binadamu na wakapita katika mishipa ya damu kama vile maji yanavyopita katika mishipa hiyo.
na katika dua yao ya tatu kuwa sisi tusiwaone lakini wao watuone,na kama kuwaona sisi mpaka watake wao wenyewe ndiyo tuwaone nayo pia ilifanikiwa kukubaliwa lakini walipewa masharti maalum katika hili.....
kama nilivyotangulia kueleza uadui uliojiri kati ya majini na binadamu ulikuwa ni mkubwa mno kwa kupokonywa kwao mamlaka hivyo wakaona njia pekee ya kumkomesha binadamu ni kueneza uadui baina yao,na kuleta madhara mbalimbali kwa binadamu hawa
shekh Al uthaimin anasema baadhi ya majini baada ya kufahamu uadui uliotokea baina ya baba wa binadamu wote ambaye ni adamu alaihi ssalaam na baina ya baba wa mashetwani yaani Ibilisi laanatullah walishikwa na kibri na wivu katika hali kama hiyo wakaanza kutafuta njia ya kumpa nusura baba yao ibilisi hivyo wakaanza kubadilika na kuingia katika miili ya wanadamu na wanapoingia huleta madhara makubwa sana....
ili kujijua kama na wewe ni muathirika wa uadui huu soma post yangu inayoelezea DALILI ZA MTU MWENYE JINI.