Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 27 Mei 2018

UHAI,KIFO,MWILI NA ROHO

Uhai ninini?
Uhai ni muunganiko wa mwili na roho...
Hivi viwili kimoja kikiwa kinaonekana na
kingine kikiwa hakionekani, ungano lao
kwa usahihi wake ndio huleta kitu kinaitwa
UHAI
Tibazetu.blogspot.com
2. Kifo ninini?
Kifo ni hali ya kukoma kwa uhai... Kivipi?
Roho inapojitenga na kile kiunganishi
kingine kinachoitwa mwili ndio kifo
hutokea... Kifo na mauti ni kitu kimoja na
kile kile...

3.Mwili ninini?
Mwili ni kibebeo, ni jumba ni kasha... Hapa
ndio roho huja na kukaa ili kukamilisha
tendo la uhai.. Na hivi viwili vikiwa pamoja
ndio hutengeneza kitu kinaitwa nafsi au
utambulisho...

tibazetu.blogspot.com
4. Roho ninini?
Roho ni nishati... Roho haionekani, haina
umbo, haina sura, haina harufu... Hivyo
vyote ni vya mwili... Lakini ili viweze
kufanya kazi vinahitaji roho... Roho
pamoja na kuwa ni nishati lakini katika na
ndani ya mwili ni nishati yenye pumzi..
Hapa lazima tuelewane kuna nishati
hazina pumzi
Sasa tusonge mbele. Je kinachokufa ni
mwili, ni (nafsi) au ni roho?
Kwa tafsiri iliyozoeleka ya kibinadamu
kinachokufa ni mwili... Kwa nini mwili?
kwakuwa ndio kinachoonekana ndio
visible.. Ndio kilichoundwa ama kuumbwa..
Kila kilichoumbwa huwa na kikomo ama
ukomo wa kuwa....!!!! .... Roho ni pumzi na
ni nishati.. Nishati wala pumzi havifi
vilikuwepo vipo navitakuwepo milele....
Lakini kwa usahihi kinachokufa ni NAFSI
yaani utambulisho wako wewe... Na ndio
maana tunaambiwa kila nafsi itaonja
MAUTI... haisemwi mwili wala roho bali
nafsi... kwahiyo hata tunapofanya ibada na
chochote kinachohusika na wafu tunadili
na nafsi na sio mwili wala roho!
Najua fika utasema mbona kuna roho
mfu? Kiuhalisia hakuna roho mfu.. Ufu wa
roho ni ile hali ya mwili kutengana na roho
na hapo ndio tunapata tafsiri mbili moja
ikiwa sahihi na nyingine ikiwa sio sahihi...
Sahihi ni mwili mfu kwakuwa baada ya
kutengana na roho wenyewe huendelea
kuharibika kuoza na hatimaye kupotea
milele
Kinachobaki ni nafsi utambulisho ambayo
haipo tena bali historia yake!
Roho hubaki ikisubiri kiama ama kuingia
kwenye utaratibu mwingine ama kugeuka
mzimu......

Tibazetu.blogspot.com