Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Alhamisi, 17 Machi 2016

ZIJUE ATHARI ZA UCHAWI WA GHASKHINI KATIKA KAZI ZETU ZA KUJIPATIA KIPATO

Habari ya mchana ndugu mpendwa mfuatiliaji wa makala zetu mablimbali zenye kukupa ufahamu juu ya maradhi mbalimbali yanayoizunguka jamii yetu,iwe ni maradhi yanayotokana na nmazingira yanayotuzunguka au viumbe wenzetu wachawi na majini,leo tutauzungumzia uchawi wa GHASKHINI

Huu ni katika uchawi hatari sana hasa unapokusudiwa kuelekezwaa kwenye upande wa kazi ya mtu fulani ili kumuharibia asifanikiwe kwani uchawi huu una nguvu kubwa sana ya kusafiri haraka na kumuathiri aliyekusudiwa ndani ya muda mchache saana na hatimaye kusababisha madhara makubwa kwa mkusudiwa na hata waliopo pamoja nae kazini hapo.


JINSI WANAVYOFANYA UCHAWI HUU
~pindi wachawi wanapomkusudia kumfanyia fulani bin fulani uchawi huu basi kama kawaida inachukuliwa miti miwili inayotumika sana katika kazi hizi HANJARI NA FAIJAR baada ya kupata unga wa miti hyo miwili wanachanganya na mafuta ya mwili wa mtoto mchanga aliyefariki na kuzikwa

~wakishamaliza kuchanganya uchafu huo wakiwa uchi kama walivyozaliwa wanauweka mchnganyiko huo mbele yao na kuanza kusema maneno yao kwa wachawi wenzao kutoka katika jamii ya majini waliohasi ili wawasaidie kutekeleza kinachofanywa hapo(maneno hayo tuyaache tuu kwenye mabano kwa faida yetu sote)

~Basi wakiwa wanaendelea na kutamka maneno hayo yaliyojaa kufru nzitonzito na uchafu wa kila aina ghafla inaanza kutoka mionzi mfano wa moshi kwenye ule mchanganyiko wao na hapo wanautuma ''nenda kwa fulani bin fulani na ukamuharibie kazi zake au jambo lolote lingine wanalolikusudia wachawi hawa waliolaaniwa 

~Basi mionzi hiyo inasafiri moja kwa moja na kwenda mpaka kwenye ofisi,kibarua,biashara au kazini kwa fulani na kujikita hapo

~Basi ndani ya muda mfupi inabadilisha mazingira ya kazi hiyo yote mazuri yanageuzwa kuwa mabaya zitaanza kuzuka chuki mara huyu anamchukia yule,watu wanafukuzwa kazi bila sababu za msingi,ukiingia kazini unaona ovyo tuu,unatamani kuacha kazi uliyoipata kwa shida bila hata sababu za msingi,biashara inakuwa ngumu ghafla,kufilisika  na mionzi hiyo inafukuza kila mtu ambaye anaonekana kuwa na manufaa na wewe katika kazi yako

~Pia uchawi huo unapomuingia mtu mwilini unamshawishi mtu huyu kutumia kipato chake kwa matumizi ya kipuuzi na kushtuka pale pesa zinapokwisha,mfano unaweza kupanga malengo''nikipokea mshahara wangu ntanunua nyumba au kitu fulani lakini unapopata tuu zile pesa unajikuta unatumia mambo mengine mengine ya kiupuuzi au yatazuka magonjwa na matatzo amabayo utashughlika nayo na pesa ikiisha ndyo utakumbuka kuwa ulichokipanga hujakitimiza na kila siku mchezo ndyo huo huo.,

UTAMJUAJE MTU ALIYEATHIRIWA NA UCHAWI HUU

1.Mtu aliyeathiriwa na uchawi huu huwa ni mwenye hasira za ajabu na hupenda kutoa maamuzi ya kijinga kwa nmsukumo wa hasira zitokanazo na uchawi huo

2.Mtu aliyeathiriwa na uchawi huu huwa siku zote kazi zake zinayumba  hafanikiwi na haziwez kuwa sawa

3.Mtu aliyeathiriwa na uchawi huu huwa ndoto hizi ndiyo ndoto amabazo atakuwa anaziota sana usingizini mwake
a)kuota anafukiwa kaburini(kuzikwa)

b)kufukuzwa na mnyama mkali

c)unauliwa

d)umepanda mnyama mkali na unatembea sehemu za jangwani


TIBA YA UCHAWI HUU
ZIPO NJIA NYINGI ZA KUTIBU UCHAWI HUU KUTOKANA NA UTAALAM WA TABIBU LAKINI NJIA NYEPESI NI


 ~CHUKUA MAJANI YA MZAITUNI YASAGE

~SHAJARATUL MARYAM

~HABBAT SAUDA YA UNGA

~QWISTWI 

~ALQISUS

~HABBAT RISHAD

CHEMSHA SANA MCHANGANYIKO HUO KWENYE MAJI MENGI

 ISOMEE DAWA HIYO AYA ZA ''KUBATILISHA UCHAWI''

NA UTUMIE KWA KUNYWA NUSU GLASS KUTWA MARA3 KWA SIKU 16 AU ZAIDI MWISHO 21 HUKU UKIOGA DAWA HIYO KUTWA MARA1 MUNGU AKIPENDA UTAKUWA SAWA.