Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 29 Machi 2016

JINSI NDEGE AINA YA BUNDI ANAVYOSINGIZIWA KUHUSIKA NA UCHURO

Habari zenu wapendwa watembeleaji wa blog yetu hii ya tibazetu.blogspot.com natumai mu wazima wa afya na mnaendelea vyema na harakati zenu za kila siku katika ujenzi wa taifa letu,na wale ambao wamejaaliwa maradhi muwe na subra mungu atawaondoshea aamin.

Ndege aina ya bundi watu wengi wamekuwa wakimuweka kwenye kundi baya la kumdhania kuwa moja kwa moja hutumika kwenye shughli za uchawi,lakini sivyo ilivyo kuwa kila bundi hutumika kwenye mambo hayo kama wengi wanavyoamini ila mchawi anaweza kumtumia mnyama yoyote anayemudu awe paka,mbwa,kuku n.k

UCHURO NI NINI?
Uchuro ni ishara zinazojitokeza endapo kuna jambo baya linataka kutokea  au likishatokea kama vile msiba lakini katika mazingira ya imani za  kishirikina.mfano mtu anapomuona bundi ametua au analia juu ya nyumba yake au sehemu yoyote katika mazingira ya nyumba yake basi watu wanahisi ni ishara ya msiba au kupata habari za msiba au kama kuna mgonjwa hospital basi watu wanaamini ameshakufa mpaka ukapatikana msemo wa kiswahili ''NDEGE WOTE WALIE LAKINI AKILIA BUNDI UCHURO'' ila mara nyingi kwa wanaoamini hivi baada ya kumuona bundi akilia huwa yanatokea kweli inakuwaje sasa??

Sasa hapa maswali ya kujiuliza kwa wale wanaoamini bundi akilia kwenye nyumba yako ni msiba mfano wewe unaishi dar es slaam na nyumbani kwenu ni dodoma kijijini,sasa akaja bundi akalia karibu na nyumba yako na ikawa ni kweli msiba,jee huyo bundi atakuwa ametokea dodoma na baada ya kujua umefiwa ndiyo akaleta taarifa???au bundi huyu anaishi hapohapo dsm ila ameletewa taarifa ya kifo cha ndugu yako na jamaa zako ili akujulishe wewe???au bundi wenzake wa dodoma wamempa taarifa kwa kumpigia simu???anajuaje sasa???

HUU NDIYO UKWELI KUHUSU MCHEZO HUU WA MASHETANI YANAVYOFANYA

Kwanza tunapaswa kujua kwamba familia yoyote yenye kuamini mambo haya ni kwamba  shetani hupenda hiyo mila aliyoipandikiza isiondoke kwenye ukoo na waendelee kurithiana.

Endapo kama kuna mmoja amehama kutoka maeneo au kijiji hicho cha watu wenye imani za namna hiyo na kama kimetokea kifo basi mashetani husika wa eneo hilo wanatambua sababu tunaishi nao kwenye mazingira yetu na wanatuona ingawa sisi hatuwaoni,wafiwa wanapolia na kuomboleza mashetani hao wanawaona na kuwasikia.

kinachofanyika ili kuifanya imani hii isipotee basi anatumwa shetani mmoja kwenda kumtafuta fulani ambaye hayupo pale na hajapata taarifa ya msiba bado,basi shetani hufanya msako mpaka anahakikisha anampata huyo mtu aliyehama kule kwenye imani hizo na wanaenda mpaka nyumbani kwake na shetani huyu anajigeuza ndege aina ya bundi kisha anaanza kulia kama kawaida ili kumshtua mtu mwenye imani hii kuwa kuna kifo kimetokea na punde tuu ndugu wa yule jamaa wakimletea taarifa kamili  za msiba jamaa yao huyu aliyemuona bundi hushtuka na imani hiyo inazidi kujikita moyoni.

UFAFANUZI JUU YA HILI
~Usishangae kwani mashetani wana kawaida ya kumfuatilia mtu wao endapo atahama kutoka sehemu moja mpaka nyingine.

~mashetani wana uwezo wa kujigeuza umbile lao,hivyo si ajabu kuigiza umbile na sauti ya mnyama au ndege yeyote

~mashetani wana umoja wa hali ya juu hivyo watahakikisha tuu lazima mtu wao wampate popote alipo.

kwahivyo ndege bundi hana makosa hii ni michezo ya mashetani kuendeleza imani hizo mioyoni mwa watu wao wanaoamini wakimuona bundi analia ni msiba.

kwa maoni,tiba na ushauri wasiliana nasi
0653 532036
0764 995259
tibazetutz@gmail.com