Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 6 Machi 2016

JINI MWENYE MADHARA MAKUBWA SANA KWA BINADAMU NA SILAHA YA KUPAMBANA NAYE

Siku1 katika masiku mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake alikuwa anasafiri akiwa na Malaika Jibriil,na alifika sehemu inaitwa Baitulrrahmi huko Jerusalem mara akamuona afriti katika majini.Jinni huyu alikuwa anamfuata Mtume s.a.w huku akiwa ameshika kijinga cha moto na hapo ndipo mtume s.a.w akafundishwa dua maalum ambayo akiisoma dua ile yule shetani ataangukia pua yake na kile kijinga cha moto kuzimika na hatimaye ndiyo mwisho wa jini hili lenye nguvu.

Malaika Jibriil a.s ndipo alipoanza kumuelezea mtume Muhammad s.a.w kuhusu jini huyo TAABIA kama hivi:

''Mfalme Suleiman Bin Daud siku moja alikuwa amekaa kwenye kiti chake cha ufalme hali ya kuwa upepo umembeba na upande wa kulia kwake kuna binadamu,kushoto kwake kuna majini,mbele yake kuna jeshi imara la ndege na nyuma yake kuna mashetani(shetani ni jini aliyehasi)

Basi Mfalme suleiman alikuwa akiwahukumu kwa haki na uadilifu huku akiwatuma na kuwaamrisha kufanya yale mambo yanayomridhia Mwenyez Mungu.

Mwenyez Mungu mtukufu akampa Idhni Nabii Suleiman awakamate Mashetani wote(majini wale waliohasi amri ya Mungu)na awafunge jela ili wasiweze kuendelea kuleta madhara kwenye maisha na afya za binadamu basi walikuja mashetani wote kasoro shetani mmoja hakuonekana pale katika kundi la mashetani waliokamatwa naye si mwingine ni huyu shetani tunayemzungumzia  TAABIA

Wanajeshi wakasema''Ewe nabii mbona hatumuoni hapa kwenye kundi shetani Taabia wakati yeye ndiye anayeongoza kwa kusababisha madhara makubwa sana kwa binadamu?"

Nabii akawajibu''Mleteni huyo shetani Taabia haraka sana,yaani kabla hajamaliza maneno hayo wale wanajeshi walienda na kurudi wakiwa wamemkamata na kumfunga pingu na minyororo ya chuma

Nabii Suleiman akamtazama sana yule jini kisha akaanguka na kumsujudia MWENYEZ MUNGU MTUKUFU ALIYEUMBA VIUMBE VYOTE na alipoinuka kwenye sijda akamwambia yule shetani ''sijawahi kuona kiumbe mbaya kama wewe na sijawahi kuona kiumbe mwenye mandhari mbaya  na chafu kama wewe''sasa nataka unifahamishe wewe ni nani?

wakati huo jini huyu Taabia alikuwa amesimama akiwa amekunjua mbawa zake kubwa,ana manywele machafu yametimukatimuka huku anapigapiga ardhi kwa miguu yake iliyofungwa minyororo lakini pamoja na hivyo ardhi yote ya pale ikawa inatikisika kwa kishindo kama kuna tetemeko la ardhi na anatoa sauti kali ambayo inasababisha mpaka miti inakatika yenyewe kwa ukali wa sauti hiyo.

Wakati wakiwa bado wapo hapo Malaika Jibriil akasema''Ewe Nabii wa Mungu mchukue huyu shetani na uende naye katika ardhi ya mbali umchome moto mpaka uhakikishe amebakia majivu na uyachukue majivu hayo uyarushe hewani yachukuliwe na upepo mkali yakatupwe katika ardhi ya mbali.Basi hapo yule Shetani akadakia na kusema''Ewe Mjumbe wa Mungu usinichome mimi kwa moto kwani Mwenye mamlaka ya kuadhibu adhabu hiyo ni mmoja tuu Mwenyez Mungu  Mtukufu,mimi ntakueleza jina langu,na mambo yote machafu nnayoyafanya kwa binadamu na ntakufahamisha kitu ambacho ukifanya mimi pamoja na kabila langu na taifa kwa ujumla hatutaweza kumdhuru binadamu mwenye kufanya kitu hicho.

Basi Nabii wa Mwenyez Mungu Suleiman Bin Daud akamuadhibu vya kutosha na baada ya adhabu huyu jini akaanza kujieleza:

''Mimi naitwa Shetani Taabia,mimi ndiye ninawafanya watu wayakimbie majumba yao''(mfano utakuta mtu amejenga nyumba yake mpya,nzuri lakini ukimtajia kwenda kuishi humo hataki hata kuskia kutokana na vituko vya jini huyu maluuni)

''mimi nawasababishia binadamu matatizo mengi na napenda kulala katika miili ya watoto wadogo na kuwasababishia kuwa kama watakufa muda wowote hali ya kuwa wapo hai kwa maradhi ya kuingia na kutoka''(anapomuingia mtoto jini huyu humtia maradhi mpaka wazazi wanaweza kukata tamaa na kuona kama mtoto wao atakufa muda wowote na akipata nafuu hurudi katika hali ya kawaida kisha humrudia tena,hayo yote ni mateso ya shetani huyu)

"pia mimi napenda sana kuwatia watu ufukara na kuwaporomosha wenye mali wakawa maskiiini''(hapa ndyo unakuta jamaa alikuwa tajiri lakini akiingiwa na jini huyu hufilisika bila kujielewa na kurudi kwenye ufukara wa kutisha)

akaendelea kueleza jini huyo
''pia mimi napenda kuufurahia usingizi wangu kwa kulala  kwenye miili ya wanawake wenye hedhi.Mwanamke atakayeingwa na jini huyu anayependa kulala kwenye miili ya wanawake wanaobleed atakuwa na hali zifuatazo
~Mwanamke huyu atapata ugumu wa kizazi na hata akienda hospital kufanya vipimo ataambiwa yupo sawa hana tatizo

''pia mimi hupenda kuwaingia wanawake wajawazto na kuharibu mimba zao mara kwa mara na hata  wakati wa kujifungua na kuwasababishia shida wakati wa kujifungua pamoja na kutengeneza kifafa cha uzazi

Hayo ni baadhi tuu ya madhara ya shetani huyu ambayo aliamua kuyaeleza mwenyewe kwa ulimi wake na yapo mengine mengi lakini mwisho wa siku baada ya mazungumzo hayo na Nabii wa Mungu Suleiman Bin Daud jini huyo alitoa maneno ambayo ndiyo silaha ya kuwachapa majini hawa aina hii ya Taabia na majini wengine ambao wapo katika ukoo mmoja kama vile Ummu subiani,Ummu muldami,shalwuush,Abluush na wengineo 

JEE MANENO HAYO NI YAPI?
Maneno hayo ndugu mpendwa msomaji yanapatika katika kitabu cha quran tukufu ndani ya surat Bani Israel aya ya 80-81-82

Ukisoma aya hizo basi kwa uwezo wa Mungu jini huyu na ndugu zake katika ukoo wao hawatoweza kukudhuru na chochote.

Na ikiwa mtu ameingiwa na jini huyu yachukuliwe majani mabichi ya mkunazi yatwange na yatiwe kwenye maji safi yasomewe aya hizo na mgonjwa anywe na kuoga basi atapona na majini hayo yatatoka na kukimbia.

kwa tiba na ushauri usisite
0653532036
0764995259
tibazetutz@gmail.com