Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 29 Februari 2016

NAMNA YA KUMFANYIA MGONJWA WA MASHETANI VISOMO VYA RUQYA NA MAANDALIZI YAKE

Sehemu ambayo inaandaliwa kwa ajili ya kumfanyia mgonjwa visomo vya ruqya ni lazima iwe ni sehemu ambayo haina kitu chochote cha kishirikina mfano hirizi,tarasimu,chupa zilizozikwa ardhini,kutundikwa nk 

pia panatakiwa pasiwe na mapambo ya sanamu za kuchonga,kufinyanga,midoli,au picha za kuchora za viumbe hai au picha za kamera wala pasiwepo mtu kati yenu ambaye amevaa vitu vya kishirikina mwilini mwake 

wote muwe na udhu kamili,yatolewe mawaidha kwanza kabla ya kuanza dua,msomaji aombe ulinzi na wepesi kutoka kwa M/mungu kwani ajue anajiandaa kuingia kwenye vita na adui asiyemuona 

anayefanyiwa dua asione hasara kumpa sadaka msomaji kwani jukumu hilo ni kubwa sana na sadaka hufanya mambo kuwa mepesi kwa uzito wa sadaka yenyewe

asitie nia "sitoi sadaka hadi nipone''kwani hiyo sadaka halipii ''kupona''bali huduma anayofanyiwa, na kupona ni kazi yake Mungu

Wote muelekee kibla na msomaji aweke mkono wake wa kulia na aanze kumsomea mgonjwa aya hizi

1.surat lfatha x7

2.albaqarah aya ya 1-5 x7

3.albaqarah aya ya 102x7

4.albaqarah aya ya 163-163

5.albaqarah aya ya 225

6.albaqarah aya ya 285-286

7.Aal imrani aya ya 18-19

8.Al aaraf aya ya 54-56

9.Al aaraf aya ya 117-122

10.yunus aya ya 81-82

11.twaha aya ya 69

12.Al muumin aya ya 115-118

13.Asswaffaat aya ya 1-11

14.Ahqaaf aya ya 29-32

15.Arrahmaan aya ya 33-36

16.Al hashri aya ya 21-24

17.Al jinni aya ya 1-9

18.Ikhlaasw yotex3

19.Al falaq yotex3

20.Annaas yotex3

utasoma aya hizo na kuzirudia mara3 na isipungue muda wa siku7 mfululizo

na ikiwa jini huyo atapanda na kuwa mbishi basi mlinganie sana na umsomee visomo vya adhabu ama vitisho vya qiyaama kama vile surat yaasin,surat annabai aya ya 21-30,surat azzilzalah,alqaarih,attakathur,alkaafirun,alfiil,na surat lmasad

MUHIMU
Msoma ruqya anatakiwa awe mchamungu na asifanye maasi kwani mashetani anaowaunguza hawatokubali kumuacha watamfuatilia sio chini ya miez3 ili wapate nafasi ya kumkomesha hivyo asikose kufanya dua za kinga asubuhi na jioni na nyiradi kujikinga na viumbe hao.