Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 9 Februari 2016

TIBA YA KUONDOA KWIKWI

Kwikwi ni ugonjwa ambao kuna baadhi ya watu wengi huudharau na kuona kama ni hali ya kawaida tuu na hauna madhara yoyote,lakini tunapaswa kujua kwamba huu ni ugonjwa unaosumbua sana pia kuna watu kadhaa ambao hufariki kutokana na ugonjwa huu.

Zipo njia za asili ambazo zinaweza zaikaondoa tatizo hilo pindi linapokukuta



        ASALI NA KITUNGUU THAUMU


Asali na kitunguu thaumu huweza kuondoa tatizo hili
\
~Saga kitunguu thaumu kiasi cha punje15 na uchanganye na asali kijiko1 kisha kula kutwa mara3


                        ZAMBARAU

~Hili ni tunda zuri kwa kuliwa na lina ladha nzuri,lakini wengi hawajui kama mzizi wa mti huu ni dawa nzuri katika kuondosha tatizo hili la kwikwi
                         MATUMIZI
~Chukua mzizi wa mzambarau kisha uchemshe vyema hadi uive vizuri,kunywa kikombe cha kahawa kutwa mara 2 basi utaondokewa na hili tatizo

KOKWA ZA ZAMBARAU

~Anika kokwa za tunda la zambarau juani zikauke hadi ziwe kavu kabisa kisha zitwange upate unga.

~unga huu ni tiba ya kwikwi ikikupata bwia unga huo mdomoni na uumeze kisha ushushie na maji safi ya kunywa utapona inshaa Allah