Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Ijumaa, 7 Julai 2017

tiba kwa mtoto aliyechelewa kuzungumza

Tangu mtoto anazaliwa hujaribu kuwasiliana na wanaomzunguka. Kulia ni lugha ya kwanza anayoitumia mtoto kuwasiliana na wengine. Hulia kuonesha kutokuridhishwa, wasiwasi, maumivu au hata kutafuta kusikilizwa. Lakini kadri mtoto anavyozidi kukua, mbinu ya kulia kama namna ya kuwasiliana hupungua na mtoto huanza kujifunza kuwasilisha hisia zake kwa kutumia sauti zisizoeleweka. 

Mama akimsaidia mtoto kujifunza  PICHA: readingrockets.org
Ni kawaida kwa watoto wa miezi miwili hadi sita kucheza kwa kutoa sauti kama Brrrr-brrrrr! Da-da-da-da! zinazoonesha furaha na sisi wazazi wakati mwingine huziigiza sauti hizo kama namna ya kuonesha furaha yetu tunapokuwa nao.

Mpaka anapofikia umri wa miezi sita, mtoto huanza kujifunza lugha ya mama yake hatua kwa hatua. Kwa mazingira yetu kuna maneno ya awali kama ‘mama’, ‘dada’ ambayo kwa kawaida mtoto huanza kuyatamka kama ishara ya kuanza kuongea.

Kadri anavyoendelea kusikia maneno kwa watu wanaomzunguka, ndiyo anavyoongeza maneno anayoweza kuyatamka siku kwa siku. Katika umri wa miaka mitatu na minne mtoto huiga maneno mengi zaidi hasa yale anayoyasikia yakitamkwa mara kwa mara katika mazingira yake.

Wakati mwingine neno moja kwa mtoto humaanisha zaidi ya jambo moja. Mfano neno ‘mma’ laweza kuwa na maana ya ‘mama’, ‘maji’, ‘njaa’ na kadhalika. Ni kama vile mtoto huonekana kuelewa vitu vingi zaidi ya vile anavyoweza kuvitamka kwa maneno yake.

Katika umri wa miaka mitano na sita mtoto huanza kumudu lugha na huwa mwongeaji. Hupenda kusimulia yale anayokutana nayo na kuuliza maswali mengi. Kadri anavyopata msaada kwa wanaomzunguka, mtoto hujifunza msamiati zaidi. Baada ya miaka sita, mtoto huwa bingwa wa lugha na huweza kuitumia kwa ufasaha katika kufikiri asiyoyaona.

mtoto wako anapokuwa  ana matatizo ya kuchelewa sana kuzungumza basi tumia dawa hizi zitamsaidia


🌴TIBA KWA MTOTO KUCHELEWA KUZUNGUMZA🌴
Tumia mojawapo kati ya hizii ---------~~
     🌹 TIBA No.1🌹
         🍃MAHITAJI🍃
👉 Udil-karaha 
👉 Lozi tunda 
👉 Sukari ya mawe 
          Hakikisha dawa zote hizo ni za unga na uzichanganye kwa ujazo sawa .
         Chukua kijiko cha chai cha dawa hiyo changanya na kijiko kikubwa cha asali kisha ale ,  fanya hivyo kwa muda wa siku 30.


          🌷TIBA No.2🌷
🌺Msugulie ZAATARI  kwenye ulimi mpaka atoe mate kutwa mara mbili siku 14.


           🌲TIBA No.3🌲
🌺Changanya AKIR-KARH na siki kisha chemsha :; 
    Asukutulie kutwa mara mbili siku 14 ;, 

     Hii ni nzuri hata kama mtoto ulimi umelegea utakaza.