Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumamosi, 17 Juni 2017

Karibu kwenye lango kuu la kuzimu pangani mkoani Tanga



Habari zenu wafuatiliaji wa tiba zetu

katika mada yangu iliyopita kuhusu malango ya kuzimu yanayopatikana hapa Tanzania nilizungumzia lango kuu la kuzimu linalopatikana Upanga Dar es slaam.bonyeza hapa usome zaidi https://tibazetu.blogspot.com/…/wajue-majini-12-wanaopatika…
leo nimeona niwaelezee kuhusu majini 12 wanaopatikana katika lango kuu la kuzimu lililopo huku kwetu pangani Tanga
LANGO LA KUZIMU LA PANGANI, TANGA
Pangani ni mmoja ya miji ya zamani sana, upo kiasi cha kilomita 35 kutoka Handeni, kama una uwezo wa kuchapa mguu sawasawa itakuchukuwa muda wa masaa matatu hadi manne kufika Pangani. Maendeleo ya mji huu yamedumaa, sawasawa na miji mingine mingi iliyokaliwa na Waarabu, licha ya kuwa na vivutio vingi vya utalii.
Ushirikina ndiyo shughuli kubwa katika mji huu, na hapo lipo lango la kuingilia kuzimu linalojulikana kwa jina la RAJUNI, lango hili lipo ndani ya bahari ya Hindi. Na linahudumiwa na majini makali kumi na mawili yafuatayo. (inashangaza sana kuwa malango yote ya kuzimu yanahudumiwa na majini kumi na mawili)

1. Shadirun hili ni jini linalosimamia magonjwa ya ngozi, na fungus zisizosikia dawa na zinazowasha sana hasa katika sehemu za siri.

2. Fadhan ni jini wanalotumiwa sana na wachawi kutambua kinga ya mtu, kabla ya wachawi hawajaenda kumfanyia ulozi. Hutumwa sana kwa walokole na huweza kutambua walokole feki na walokole wasioingilika.

3. Baraji ni jini linalosimamia uvivu hasa kwa wanawake. Jini hili likitumwa kwa mwanamke anakuwa mvivu kweli kweli kwa kazi za nyumbani hadi kitandani.

4. Shamsu ni jini linalo vaa umbile la binadamu. Utakuta msichana ni mzuri sana kwa sura na tabia lakini haolewi. Akitokea mvulana kumchumbia hili jini humwingia msichana na kumvika sura bandia, mvulana anapomtizama msichana anachanganyikiwa kwani anaona siye yule aliyekuwa anamtaka, hivyo anapigwa chenga hadi uchumba unavunjika. Akijitokeza kijana mwingine hali huwa ni ile ile ya kuachwa. Wasichana wengine hufunikwa kwa sura bandia kiasi kwamba tangu azaliwe hajawahi kukutana na mvulana walao wa kumtakia neno nakupenda.

5. Amri ni jini linalosimamia hasira. Utakuta mtu anakuwa na hasira hadi anatetemeka na mapovu yanamtoka mdomoni.

6. Tahimu anashughulika na kutambua nyota za watu, kisha wachawi huzichukuwa na kufanyia biashara.

7. Tajirin hili ni jini linalosimamia utajiri. Masharti ya kulimiliki ni lazima uwape mtoto wako wa kuzaa au mke wako apooze upande au ufanye mapenzi na mama yako mzazi. Kisha ni lazima usaini mkataba wenye masharti magumu sana kama usilale kitandani, usipande gari, usile aina ya vyakula nk.

8. Al Taliki hili ni jini la kupoteza watu. Kama kuna watu wanamtaka mtu fulani, wachawi hutuma hili jini nalo huvaa mwili wa binadamu na kwenda eneo au sehemu anapoishi huyo mtu. Likimwona huwita kwa vidole na watu wengine wanakuwa hawamuoni isipokuwa mlengwa peke yake, kisha huanza kumfuata jini kwa nyuma,jini akikimbia na huyo mtu naye hukumbia hadi anamfikisha kwa wachawi.

9. Naruju ni jini linalosimamia lugha, wapo wanao nena lugha kwa kupagawa na majini na wapo wanao nena lugha kwa nguvu ya Mungu ambayo inawapa taabu sana kuzimu kwa moto unaounguza.

10. Janjatus ni jini linalotumwa kuwafanya watu walale usingizi mzito wakati wa adhana na wakati wa mahubiri kanisani.

11. Riaru jini hili likimwingia mtu anataka afanye kila kazi peke yake.

12. Zaituni ni jini linalosimamia watoto wa kike kutembea kwa maringo na mikogo na umalaya mwingi.