Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 17 Novemba 2015

NJIA KUU5 ZA KISHERIA ZA KUMUUNGUZA JINI NA KUMUUA KABISA


Hizi ni njia ambazo kama zitatumika vizuri kabisa huweza kumtoa jini wa aina yoyote mwilini mwa mgonjwa kwa kumuunguza na kumuua kabisa kama atakuwa ni mbishi na asiyetaka kutoka mwilini mwa mgonjwa.

NJIA YA KWANZA
Katika njia hii mgonjwa anatakiwa atie udhu vizuri akae kitako na aelekee upande wa kibla kisha

1.asikilize quran surat baqara yote kwa kikao kimoja kwa muda wa siku3

2.mgonjwa asikilize quran yote kwa kikao kimoja kwa siku moja

3.mgonjwa asikilize aya za adhabu zote kwa kikao kimoja  na azirudierudie kila zinapomaliza kusoma



NJIA YA PILI
Katika njia hii mgonjwa asomewe visomo hivi hali ya kuwa yeye na msomaji wawe na udhu na waelekee upande wa kibla

1.asomewe adhana kama ya kuitia kwenye swala mara 7

2.asomewe surat Sswaaffaat mara 7   

3. asomewe Surat ljinni mara 7

4.Surat qaaf mara 7

5.Surat raad mara 7

6.Surat ttwaaraq mara 7



NJIA YA TATU
Katika njia hii msomaji anatakiwa ayasomee maji safi surat buruuj na iandike sura hiyo kwenye kitambaa kisha ayachukue maji hayo ampige nayo mgonjwa usoni hali ya kuwa anasoma kwa wingi sura hiyo halafu chukua hicho kitambaa kiunguze moto na umnusishe mgonjwa avute ule moshi jini huyo atatoka mara moja na km ni mkaidi basi atadead na kuangamia kabisa.



NJIA YA NNE
Utamsomea mgonjwa surat yaasin mara2 na surat jinni mara3 kisha utazirekodi kwenye kanda awe anasikiliza mgonjwa mfululizo kwa siku 7 au 14



NJIA YA TANO
Katika njia hii utamuwekea mgonjwa mkono wako wa kulia kichwani na wote muwe na udhu na umsomee 
 1.msomee swalatu ibrahimiyya mara 11
2.surat fatha mara 11
3.soma tena swalatu ibrahimiyya mara11
4ayaturkursiyyu mara 11
5.soma tena swalatul ibrahimiyya mara11
6.soma surat kaafirun na ikhlaasw zisome pamoja mara 11   
7.soma tena swalatul ibrahimiyya mara 11
8.soma aya za kubatilisha uchawi mara 11
kisha maliza kwa kusoma swalatul ibrahimiyya mara 11