Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 25 Agosti 2015

mjue jini mwenye mabawa

~Kwanza inakupasa ufahamu kwamba kama tulivyo aina mbalimbali za bin adam pia ndivyo walivyo majini,lakini cha kustaajabisha ni kuwa  tofauti za majini kwa majini zinaachana mbalimbali sana ukilinganisha na tofauti za maumbile kati ya mwana adam na mwana adam

~Wana adam tunatofautiana rangi,kimo,umri na hata lugha[makabila]na hata kukawa na wazima na wenye upungufu wa viungo[walemavu].Jambo hili ni tofauti kwa upande wa majini kwani pamoja na tofauti zote hizo tulizonazo na hata majini wanazo ila wao tofauti zao zimezidi kimaumbile kama vile ambavyo mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotuambia "wapo majini mengine yana maumbile ya nyoka,na wengine katika umbo la mbwa mweusi,na wengine mfano wa maumbile yao ni kama bin adam,na wapo wengine wana mabawa na hutumia kwa kuruka kama ndege kwa hizo mbawa zao''..hii inaonesha kuwa kuna tofauti kubwa mno katika maumbile ya majini ingawa wote wameumbwa kwa malighafi moja.

                          SASA TUMUANGALIE HUYU JINNI MWENYE MABAWA
~Huyu ndiye miongoni mwa majini wanaopendwa sana kutumiwa na wachawi,na hii ni kwa vile yuko faster sana katika kusafirisha makombora yao kwa mtu wanayemkusudia kumfanyia ubaya wao kuliko hata speed ya chombo chochote cha usafiri unachokijua wewe.............ngoja niwafumbue macho kidoogo
Mfano mtu anaweza kwenda kwa mganga mpiga ramli ili akaangaliziwe matatizo yake,na kweli akifika hujikuta akiambiwa matatzo yake yote yanayomsumbua na kujikuta anamuamini na kumtegemea huyu mtaalam wake kuliko hata mungu.

~Mtu huyu bila kujua kumbe kuna mambo yanayofanyika baina ya mganga yule na jini huyu mwenye mbawa ambapo pindi tuu unapoanza kupanga mipango kwenda kwa kalumanzila huyu,jini mwenye mbawa anakuja na kukusikiliza na kuzijua shida zako zozote zinazokupeleka kule kisha yuleeee anakutangulia kwa mganga na anamueleza yote kuhusu wewe[mganga huyu ni lazima awe anamtumikia jinni huyo kwani jinni hamfanyii mtu kazi burebure bila makubaliano maalum].Hapo ndipo ww ukifika kwa mtaalam huyu unajikuta unaelezwa yote yaliyokuleta hata kabla haujaongea chochote.

~Jinni huyu endapo kama atamuingia mtu iwe kwa kutumwa au hata kwa kumkumba tuu mwenyewe basi ndugu ni lazima wajifunge kanga zikaze kwani balaa la jinni huyu ni zaidi ya tsunami au mafuriko.

                      ZIJUE DALILI ZA MTU ALIYEINGIWA NA JINNI MWENYE MABAWA
Hapa kabla sijakueleza dalili unapaswa ujue kuwa jinni huyu ni mjanja saaaana kwani mara nyingi
akisikia mnataja mipango ya tiba humtoka mgonjwa na kukimbia kisha mkirudi nyumbani kama kawaida anarudi humo mwilini hivyo hapa panahitaji tabibu mzuri na mwenye uzoefu wa hawa viumbe ambaye atamsomea mgonjwa na kumvuta jini popote alipo kisha kumrudisha na kuendelea kumuadhibu

*Athari zake sio za moja kwa moja bali kuna wakti zinakuwepo na kuna wakati  mgonjwa anakuwa sawa kama hajawahi kuumwa

*Mgonjwa aliyeingiwa na jinni huyu akipandisha huwa na nguvu za ajabu hata watu kumi mnaweza kushindwa kumzuia

*Kudhoofika mwili na kuumwaumwa mara kwa mara

*Mgonjwa kuhisi maumivu makali mwilini pindi anapokuwa amekasirishwa na jambo

*Mgonjwa kujihisi mwepesi na hana maumivu yoyote wakati jinni huyu kutoka kwenye mwili wake baada ya kupandisha anaweza hata akawashangaa kwanini mmemshika

*Kupoteza fahamu mara kwa mara na akifanyiwa vipimo tatizo halionekani

*Tumbo kujaa ghafla

*Joto la mwili kuwa juu sana na uso kuwa mwekundu pindi anapopanda jinni huyu

*Kuota mara kwa mara unapaa au kuona ndege wanaopaa


TIBA YAKE
~Mgonjwa afanyiwe visomo vya rukya zikiwemo aya za kuwaadhibu majini huku awe anajipaka mafuta ya HANANA...kifuani na mgongoni kutwa mara2.na akiwa ni mtoto mdogo utampaka mwili wote

mafuta haya yanapatikana
wasiliana nasi 0653 532036
0764 995259