Chukuwa kombe hilo uandike kwenye Sahani nyeupe kwa kutumia zafarani hapo kwenye jina utaandika jina la unayemtaka kumsahau kisha utapangusa hiyo sahani nyeupe iliyoandikwa kombe na kumpa utakunywa kwa siku 3 asubuhi mchana na usiku uandike siku ya jumapili saa 1 asubuhi aanze kutumia siku ya jumatatu saa 1 asubuhi.au unaweza kumuandikia kombe la sahau siku ya Alkhamisi saa 1 asubuhi kombe kisha akanywa siku ya ijumaa saa 1 Na unaweza kuandika mkononi ukaramba kwa ulimi wako. ili kombe liwe na nguvu zaidi andika kombe kwa zafarani na uichanganye na miski na marashi safi humo kwenye zafarani.