Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 18 Machi 2018

Nyota zenu leo 18.03.2018

Punda

Leo utakuwa mchovu wa mwili na maumivu ya viungo au homa hali hii inapita tu isikutie khofu, pia kuna dalili ya migogoro uliyonayo kuendelea kukusumbua kuwa mvumilivu na ujitahid kupata suluhu au msaada juu ya hilo.

Ng'ombe

Leo utajihisi mwenye bahati kwani mahitajia au maombi yako unayoyahitaji kwa mtu yatatimia, pia mpenzi wako ataongeza upendo wake kwako na marafiki zako au watu waliokutupa watakukumbuka kama ( kama hali yako sio nzuri kimaisha chemsha mjafari ubanimushtaka na magadi tumia kwa kuoga hii itakufungua zaidi

Mapacha

Matatizo ya kimaisha uliyonayo yataisha baada ya wewe kuhama au kusogea hapo ulipo na kama ni kwako umejenga basi wasiliana na wataalam ujue lakufanya. Pia kuna dalili ya kuzidi kutokuelewana na mtu anaekusaidia jitahidi kuwa mvumilivu na uzizuie hasira zako.

Kaa

Safari yoyote utakayoipata hivi karibuni inafaida kwako, pia jihadhari na mahusiano yakulazimishwa au kushauriwa na mtu (kuwa nae tu utapata hela) usikubali ushauri wa namna hii hasara itabaki kwako, licha ya kuwa unashida ya pesa kwa sasa ila usifanye dhambia au udanganyifu kupata pesa fanya ibada zaidi.

Simba

Migogoro na watu wako wa karibu itaisha, pia kuna taarifa zitakufikia za mtu kuugua au kufa usihuzunike ni njia ya kila mmoja, tegemea kutokewa na mambo ya ajabu ajabu wiki hii unaweza kuhisi ni mkosi ila ni mambo yakupita tu.

Mashuke

Maisha yako yanadalili kubwa za kimafanikio kila leo ila huyaoni na ahadi zako hazitimii kwa wakati jitahidi kufanya ibada na uwe karibu na marafiki au washauri wako wa karibu,,pia kuna safari inaweza kutokea ya kwenda mbali usiikose ni safari yenye mafunzo na faida kubwa kwako jitahid uwe msiri

Mizani

Leo sio siku nzuri kwako unaweza kukumbwa na tatizo kubwa au kijimkosi zaidi unashauriwa kutulia au kutoka na kuwahi kurudi nyumbani, pia jitahidi uwe mkimya leo usijibizane na mtu utajikuta upo katika kesi kubwa.

Ng'e

Afya yako itazidi kunawiri au kustawi na mambi yako yakimahusiano hayajatulia ila hii isikuumize inapita tu japo ya muda mrefu.

Mshale

Unatahadharishwa na tabia yako yakulazimisha mambo itakutia matatizoni, pia punguza jeuri au dharau kwa watu wako wakaribu manbo yako yatafunguka hivi karibuni jitahidi kuikubali hali uliyinayo

Mbuzi

Maradhi yanaweza kuwasumbua wanao au kusumbua ndugu yako kuwa karibu nao kuna jambo utaligundua na kujifunza, mambo yako yatazidi kufanikiwa siku hadi siku jitahidi kutoa sadaka

Ndoo

Mambo yako yakimahusiano yanaonekana kuja na sura mpya tofauti na awali pia kuna ahdi za ndoa unazozipata ahadi hizo zitatimia na zina ukweli

Samaki

Kuwa makini na mambo unayokatazwa unaweza kujikuta upo matatizoni, afya yako itastawi na kuwa vizuri mambo yako yataenda vizuri siku sio nyingi biashara zako au za mumeo au mkeo zitaanza kwenda vizuri jitahidi kuwa watu wa ibada mtafika mbali sana.