Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Alhamisi, 7 Aprili 2016

EWE MWANAUME WAJUE MAADUI 20 WA UUME WAKO


ADUI WA KWANZA
 MAGONJWA
Magonjwa ni adui namba 1 wa uume wako.
Magonjwa ya sehemu za siri, magonjwa ya mwili
kwa ujumla, na magonjwa ya wanaume kama -
tezi dume ni adui wa uume wako. Ugonjwa kama
kisukari na presha, figo na ini kutokufanya kazi
vizuri LAZIMA uume uwe dhaifu. Kuna magonjwa
mengine pia kama viupele vya ajabu ajabu huko
kwa babu pamoja na ugonjwa wa bawasiri.
MAGONJWA HAYA LAZIMA YATIBIWE HARAKA.


ADUI WA PILI
ULEVI NA SIGARA
 ulevi haufai kabisa kwa afya ya uume wako. Ulevi
unakufanya uwe mlaji wa nyama hasa nyekundu,
unakuwa sio mwepesi wa kunywa maziwa na
kula matunda, unakuwa mzembe wa majukumu
yako ya ndani, unapata vitambi, unaharibu
balansi ya homoni >> unaelekea upotevuni”
Kunywa maji ya kutosha, maji fresh ili
kuuburudisha mwili na kuondoa msongo wa
mawazo.

ADUI WA TATU 
PUNYETO NA MICHEPUKO
Watu walionishuhudia ambao walifungwa katika
minyororo ya kufanya punyeto hadi mara 6 kwa
siku, waliokuwa wanafanya hadi vyoo za ofisini na
wengine kujificha hata majumbani wake zao
wakiwa wamelala au hawapo. Vijana wa boarding
school na vyuo, mabachela na wengineo wanatoa
shuhuda zinazotisha.Punyeto imekuwa utumwa.
Wanashuhudia kupata majipu, michubuko,
msongo wa mawazo, kushuka kwa kujiamini,
wengine wameshuhudia kufika kiwango cha juu
cha kutokuvutiwa na wanawake kabisa. Kwa
kifupi punyeto huharibu vipokezi (receivers) vya
hisia mwilini na saikolojia yako ya mapenzi kwa
ujumla,kuharibu mishipa na nerve za ufahamu
katika uume na kukukosesha mawasiliano sahihi
kati ya uume na akili yako.Unaporudi kufanya
tendo la ndoa kawaida (na mwanamke) unakuwa
tayari umeathirika na inakuwa kama upo
ulimwengu wa nje ya mapenzi. Wengine
wanasema haina madhara na pia kutoa namna
nzuri ya kufanya ili usipate madhara, lakini kila
waathirika wanasema haifai….kinga ni bora kuliko tiba hivyo anza mpango wa kuacha kuacha punyeto haraka kabla hujafikia sehemu mbaya zaidi

ADUI WA NNE
MADAWA
Hapa kuna madawa ya kulevya na madawa ya
kawaida, pia madawa makali ya presha na
kisukari ni hatari kwa afya ya uume wako.
Madawa yanayowekwa katika baadhi ya makopo
ya vyakula vilivyosindikwa na mengine
yanayonyunyiziwa mashambani wakati mimea
inakuwa katika ukuaji wake ni hatari tupu.
Madawa ya kulevya nadhani wote tunayajua
yalivyonoma. Unalegea mwili mzima, uume
unajifia tu kama bamia.jenga tabia ya kutumia chakula cha asili kama dawa kuepuka magonjwa ya tabia yasikupate

ADUI WA TANO
UCHAFU WA MWILI, NGUO NA
NGUO ZA KUBANA
Nguo chafu, za mbano na zisizo za pamba
zinasababisha magonjwa ya ngozi. Pia uume
unatakiwa upate free range yaani ubembee na sio
kutulia kama jiwe. Hii inaufanya uume kuwa
active na kuwa tayari kwa kushughulika. Pia
wanaume wengi ni mabingwa wa kuvaa suruali si
chini ya siku 3 hadi 7. Wengine wanavaa jinsi
kauka nikuvae - huo ni uchafu na ni hatari uchafu
kuingia ikulu. Oga mara kwa mara fua nguo zako
hata kama wife hafanyi fanya mwenyewe, vaa
boxer chupi sio zile za chupi za V kama za
wanawake. Ukikojoa na kwenda haja kubwa
jitawaze vizuri. Kuwa msafi mwili na roho, Sasa
wengine wanafuga rasta maeneo ya Ikulu. … OK
decide yourself kama ni usafi huo au uchafu,


ADUI WA SITA
BAADHI YA CHAKULA
Hapa lazima tuambiane ukweli ivi mwanaume
unakula chips na soda kila siku unataka uwe nini
kama sio kituko, vyakula vyepesi vyepesi
visivyokuwa na nguvu vinavyokuongezea sukari
na presha mwilini achana navyo. Mwambie waifu
aachane na mapishi ya ugali uliokobolewa.
Vyakula vya kukujaza gesi tumboni havifai,
vyakula vinavonenepesha tumbo achana navyo
kabisa. Wengine wanapiga pombe kali eti
zinaongeza nguvu, at least kwa leo au kesho
“energy drinks is not a long lasting solution”.
Mara moja moja penda kutumia asali na
mdalasini, tende, matunda kwa wingi hasa yale
yenye zink kama tikiti maji, avocado, uyoga na pia
machungwa. Hakikisha unakula matunda dakika
kadhaa kabla au baada ya chakula. Usichanganye
matunda yenye acid na alkali mara moja na ukala
yaani mtindo wa cocktail, mfano chungwa lina
acid, parachichi ni alkaline (haya usiyale yote
mara moja).

ADUI WA SABA 
HOMONI KUVURUGWA
Hapa ndugu zangu pana uhusiano sana na
namba 4 hapo juu. Vyakula na madawa
tunayotumia pamoja na madawa yaliyotumika na
wakulima ndio yanaleteleza hormoni katika mwili
wako kuwa na balansi ya tofauti. Matokeo yake
hormoni zinazohitajika kuamsha vichocheo vya
kuufanya uume ufanye kazi vema zinashindwa
kuwa katika balansi nzuri na hatimaye kuufanya
uume kushindwa kufanya kazi zake kwa ufasaha.


ADUI WA NANE 
UMRI
Kadri umri wako unavozidi kwenda mbele ndivyo
uwezo wa kiafya wa uume wako unavyozidi
kupungua ingawa wanasema "old wine gets
better" Magonjwa pia ni rahisi kukuingia,
magonjwa kama tezi dume, kansa ya uume,
ubovu wa kibofu cha mkojo na pia kukosekana
kwa damu katika sehemu zako za siri.

ADUI WA TISA 
KUUCHORA UUME KWA KUTOBOA
AU KUPAKA RANGI
Wanaume wengine hujichora katika uume wao na
kuweka alama mbalimbali au majina mbalimbali.
Kwa kuwa kazi hizi katika mazingira ya kiafrica
hufanywa kwa siri basi vitogeo huwa dhaifu na
huenda vikaambukiza magonjwa, lakini pia ukisha
chora uume wako kwa kutoboa ngozi ni rahisi
kwa magonjwa kukuingia wakati ukiwa katika
harakati zako za kinyumba.

ADUI WA KUMI 
ACROBATIC AND ATHLETIC SEX
Hawa pia ni maadui wakubwa, kuna baadhi ya
wanandoa hufanya mapenzi kwa kutumia staili za
tofauti tofauti na zingine huufanya uume kupenya
kwa shida au kukunjana na hivyo kusababisha
michubuko na uvimbe katika kichwa na shingo ya
uume. Na pia wengine hufanya mapenzi muda
mrefu sana kama vile wako mashindanoni -
Jiulize unabakia salama? Starehe isiwe kero.
Pima faida ya starehe na hasara yake.

ADUI WA KUMI NA MOJA
MSONGO WA MAWAZO
Au stress huyu ni adui endapo utashindwa
kumdhibiti kwa kuwa stress husababisha milango
ya fahamu kuziba na pia kuunyima uume damu
na oxygen ya kutosha na hivyo uume kushindwa
kufanya kazi yake vizuri. Ikiwa utashindwa
kuusimamisha uume huenda ukashindwa mara
nyingine tena kwa kuwa swala hilo linaweza
kuathiri saikolojia yako ya mapenzi na hivyo
kujikuta kila wakati unashindwa wakati ki-ukweli
upo fiti. Jifunze kuwa nje ya stress kama vile
kupangilia mambo yako vizuri ya kijamii, kiofis na
kipesa (kwa sababu stress au msongo hutokea
wakati matokeo halisi yamekuwa madogo kuliko
matokeo tarajiwa na inaonekana hamna namna
ya kufanya na muda umekwisha) – Siku zote
panga siku yako vizuri na yaangalie mambo yote
kwa kutumia akili chanya. Katika kila ubaya kuna
uzuri, fuata uzuri.

ADUI WA KUMI NA MBILI
NGONO KINYUME CHA MAUMBILE,
VIDOLE NA MIDOLI
Ufanyaji ngono kinyume na maumbile ni hatari
kwa afya ya uume wako, iwe unafanya au
unafanywa yote yanapelekea kuwa na hali ya
sintofahamu mara uume unapokutana na uke. Sio
mazoea yake na sio utaratibu wa dini zetu hata
wapagani wanakataa wala sio uhalisia. Wengine
wana vimidoli vyao na vitu vinavyofanana na
hivyo. Unasinyaisha uume wako….mtoto wako anapokuwa na tabia za ajabu ajabu mkague na uongee naye mara kwa mara  sio kila siku unarudi watoto wamelala

ADUI WA KUMI NA TATU
WASIWASI WOGA NA UVIVU
WAKATI NA KABLA YA TENDO LA NDOA.
Hapa ndugu zangu hakuna maelezo mengi sana
ila kumbuka tu ya kwamba kuwa na wasiwasi na
woga kunaondoa uwezo wa damu kufika maeneo
ya uumeni hivyo kuukosesha uume malighafi
muhimu ya damu na oxygeni ili uume ufanye kazi
vizuri. Pia wewe mwenyewe mwanaume unakosa
focus (target) ya jambo unalolifanya. Kuwa
mwanaume jiamini unaweza; 

ADUI WA KUMI NA NNE
UPUNGUFU WA TESTESTORENE
Testosterone ndio homoni ya kiume inayohusika
na uundaji wa viungo vya kiume wakati mtoto
akiwa tumboni hajazaliwa na kisha kuanza
kujenga mwili wa kiume wakati kabla ya
kubalehesha na kumtayarisha kijana wa kiume
kuwa baba akisha balehe. Na baada ya hapo
homoni hii huhusika na matendo mabalimbali ya
kimapenzi na mvutano kati ya mwanamke na
mwanaume. Pia huhusika na uzalishaji na
ukomazaji wa mbegu za kiume. Homoni hii
ikipungua uwezo wa uume kufanya kazi vizuri
hupungua. Uzuri ni kwamba unaweza kuongezwa
homini hii katika mahospitali lakini pia kuna
vyakula unavyoweza kula na kuiongeza taratibu.

ADUI WAKUMI NA TANO
PICHA CHAFU, ROHO CHAFU NA
AKILI CHAFU
Uangaliaji wa picha chafu za ngono ni hatari kwa
ujumla wa saikolojia yako. Mwili wako unauwezo
wa kubadili tabia na vionjo kama utafanya hivyo
ndani ya siku 15 hadi 21. Ikiwa utazoea kuangalia
picha za ngono ambazo wataalamu wengi wa
holywood wanasema si za kweli basi unajikuta
upo katika ulimwengu ambao sio halisia. Ukija
kuonana na mkeo halisi unajikuta mwili wako wa
hisia bado upo Holywood. Akili yako imetekwa.
Huwezi fanya vizuri tena, wengine wanasema
wanatafuta apetite, lakini kumbuka apetite hii sio
ya asili baada ya muda unazoea unakuwa sugu
na huwezi tena kuwa boosted na hizo picha. Best
apetizer ni mkeo.

ADUI WAKUMI NA SITA
MWANAMKE MWENYE DHARAU NA
MATUSI
Tabia za baadhi ya wanawake zimekuwa kero
kabisa kwa uimara wa uume. Mwanamke
anakuwa mchafu kupindukia. Wengine ni kutoa
matusi mfululizo kama vile hawajaenda jandoni,
wengine ni dharau zisizokuwa na mpango hadi
wakati wa tendo la ndoa. Wanawake wengine
hawachangamki hata mwanaume ajitahidi vipi
yaani wapo wapo tu as if ni magogo. Hii ni hatari
sana. Mwanamke ni ufunguo mzuri sana kwa afya
ya mwanaume hasa kama mwanamke ameutunza
vizuri uke wake na pia kama mwanaume
hajaathirika na uoga, wasiwasi na mashaka,
magonjwa na tabia zile mbaya kama punyeto,
michepuko, ulevi na madawa ya kulevya. Wewe
mwanume unatakiwa utengeneze mazingira ya
mkeo kuwa msafi na mwema kwako, anayejituma
na ambaye ni mkweli daima. Love your wife she
will pay you back 100%.

ADUI WA KUMI NA SABA
UZITO, KITAMBI NA KIRIBA
TUMBO CHA MWANAMKE
Wanawake wengi siku hizi wana vitambi, owk
unaweza sema hii inakujaje hapa? Ukweli ni
kwamba baadhi ya shughuli za msingi za uume
zinashindikana kufanyika kwa sababu ya kitambi
cha mwanamke, ofcourse hata kitambi cha
mwanaume ni adui lakini adui namba moja ni
kitambi cha mwanamke na pili ni kitambi cha
mwanaume. Wanawake wengi wanaoshindwa
kufika kileleni wanavitambi au uzito mkubwa. Hii
inauletea uume shida sana ya kutimiza majukumu
ya kinyumba.

ADUI WA KUMI NA NANE
UKE USIOTUNZWA, uume unakuwa
bora ikiwa uke pia ni bora.
Mwanaume lazima ujiunge na mkeo
kumweka vizuri

ADUI WAKUMI NA TISA
KUKOSA USINGIZI
Kuangalia mpira kuanzia saa11 mpaka saa7
usiku, wengine wanaangalia movie huku wanakula
mirungi nabado asubuhi unatakiwa uwahi kazini. My
friend unaharibu mwili wako na uume wako
unapata stress. Ukilala mwili unapata muda wa
kurekebisha misuli, kuweka balansi nzuri ya
homoni na kurudisha hamu za mwili za kawaida
pia kuboresha kinga ya mwili. pata usingizi wa kutosha ubongo ujipange,misuli itulie na seli zizaliane

ADUI WA ISHIRINI 
TOO MUCH SEX IS HARMFUL.
Ukifanya sana ngono unahatari ya kupata
madhara yafuatayo uume kuvunjika (hauvunjiki
kama kijiti ila misuli inaumia), kuishiwa maji
mwilini, UTI, kuumiza nerve za uume, kupunguza
nguvu ya misuli na kushindwa au kuuma misuli
ya mwili. AMUA NI KIASI GANI KINAFAA
Kwa ujumla utakuwa umegundua ya kwamba
chakula ndio suluhisho la kudumu la kupambana
na maadui hawa, ingawa pia utalazimika kuwa
mwenye tabia nzuri. Endapo wakati mwingine
inakuwa ngumu kwa chakula kufanya kazi na
kuleta matokea ya haraka itakulazimu kupata
ushauri wa kitabibu kama kupata dawa za
hospitalini (kemikali) au virutubisho. Ikiwa
utapata dawa au virutubisho hivi na ukapona
huna budi kuendelea kutumia chakula bora na pia
kuwa na tabia njema kwa ajili ya kupata matokeo
ya kudumu, yenye furaha na amani.