MAJINI WA SATURN (ZOHALI) -MAJINI WA JUMAMOSI
Majini hawa huwa ni warefu, wembamba na wenye sura
ya ukatili na kutisha, wana nyuso nne ambazo kila moja
iko kila upande wa kichwa, yaani kwa mbele na nyuma
sura inakua na midomo kama ya ndege.
Pia wana sura nyeusi inayon’gaa katika kila goti. Mwendo
wao ni kama mwendo wa upepo ambao huambatana na
radi.
Alama yao ni ardhi nyeupe kuliko theluji.
Umbo lao maalum ni kama Mfalme mwenye ndevu
anaemuendesha DRAGON.
Umbo lingine ni la mtu mzee mwenye ndevu
Umbo lingine ni la Bibi kizee ambae anaegemea kitu
Umbo lingine ni la Mvulana
Umbo lingine ni la Dragon
Umbo lingine ni la Bundi (Owl)
Umbo lingine ni la Nguo nyeusi isiyo na mwili
Umbo lingine ni la Ndoano au Mundu
Umbo lingine ni la mti wa Mreteni
Hawa ndiyo majini wanaotawala siku ya jumamosi
Majini wa Sayari ya Jua (Shams) - Majini wa Jumapili
Majini wa Sayari ya Jua (Shams) wana viungo na umbo la
kati, wasiovutia na dhalimu, wana Sura nyekundu na
rangi ya dhahabu iliyochanganyikana na Damu.
Mwendo wao ni mfano wa Umeme na Alama yao kubwa
ni kusababisha mwenye kumuita kutokwa na jasho jingi
Umbo lao maalum ni la Mfalme aliyebeba fimbo ya
kifalme huku akiwa amempanda Simba.
Umbo lao lingine ni la Mfalme aliyevikwa Taji.
Umbo lao lingine ni la Malkia mwenye Fimbo ya Kifalme.
Umbo lao lingine ni la Ndege wa aina yeyote isipokuwa
wale ndege ambao wanawakilisha peponi.
Umbo lao lingine ni la Simba.
Umbo lao lingine ni la Jogoo.
Umbo lao lingine ni la Nguo ya Dhahabu isiyokuwa na mwili.
Umbo lao lingine ni la Fimbo ya Kifalme.
Umbo lao lingine la mwisho ambalo kwa kweli ni la
kutisha sana; ni lile la Kiumbe ambaye haeleweki
eleweki vizuri na ni vigumu kumuelezea ila ana mkia.
hawa ndiyo majini wanaotawala siku ya jumapili
Majini wa Sayari ya Moon (Qamar) - Majini wa Jumatatu
Majini wa Sayari ya Moon – Mwezi (Qamar) wana Maumbo
makubwa, Laini, Tulivu na rangi yao ni kama wingu jeusi.
Muenekano wao ni umbo lililotuna, Vichwa vyao vina
upara, Macho yao ni Mekundu na yanatoa Majimaji, Meno
yao ni kama ya Nguruwe Mwitu.
Mwendo wao ni kama Dhoruba kubwa Baharini. Alama yao
ni ni Mvua kubwa inayonyesha katika Mduara.
Umbo lao Maalum ni Ni la Mtu kama Mfalme anayerusha
Mishale huku akiwa anamuendesha Swala Jike.
Umbo lao lingine ni la Kijana Mdogo wa Kiume.
Umbo lao lingine ni la Mwindaji wa Kike mwenye Upinde
na Mishale.
Umbo lao lingine ni la Ng’ombe.
Umbo lao lingine ni la Swala Mdogo.
Umbo lao lingine ni la Bata.
Umbo lao lingine ni la Nguo isiyokuwa na Mwili yenye
rangi ya Kijani au Fedha.
Umbo lao lingine ni la Mshale.
Umbo lao lingine ni la Kiumbe mwenye Miguu Mingi mfano
wa Tandu
hawa ndiyo majini wanaotawala siku ya jumatatu
Majini wa Mars (Mariikh) - Majini wa Jumanne
Majini wa Mars (Miriikh) wanakuwa na Umbo refu, Mwili
Mwekundu, mchafu na hutoa harufu yenye kutia kinyaa.
Huwa wanajitokeza pia katika mwili wenye rangi
Nyekundu, Kahawia au Nyeusi. Wana mapembe kama ya
mnyama aitwaye Ayala (Hart), kucha kama za
Simba,Wanatoa sauti kama za Nyati (Mbogo).
Mwendo wao ni kama mwendo wa moto unaowaka na
Alama yao ni radi na umeme unaowaka kwa katikati.
Umbo lao maalum ni la Mfalme aliyevalia kivita akiwa
amempanda Mbweha (Mbwa mwitu).
Umbo lao lingine ni la Mwanamme aliye na silaha.
Umbo lao lingine ni la Mwanamke aliyeshikilia Ngao
kwenye mapaja yake.
Umbo lao lingine ni la Mbuzi Jike.
Umbo lao lingine ni la Farasi.
Umbo lao lingine ni la Paa.
Umbo lao lingine ni la Nguo Nyekundu isiyokuwa na
mwili.
Umbo lao lingine ni la Sufi.
hawa ndiyo majini wanaotawala siku ya jumanne
Majini wa Sayari ya Mercury (Attwarid) - Majini wa
Jumatano
Majini wa Sayari ya Mercury (Attwarid) mara nyingi
hutokea na mwili wa Kati, Baridi, Majimaji, Unyevu
nyevu. Kwa ujumla maana yake ni kusema kuwa Majini
hawa wa Sayari ya Mercury wanafanana na maumbile ya
Mercury (Zebaki).
Muonekano wa Majini hawa ni wa kuridhisha, ni
Wachangamfu katika maongezi, wana Umbo la
Kibinadamu, na wanaonekana kama Shujaa aliye na
silaha.
Mwendo wao ni kama wa Mawingu ya rangi ya Fedha.
Alama yao ni kuwa wanasababisha Vitisho, Hofu na Woga
kwa mwenye kuwaita.
Umbo lao Maalum ni la Mfalme anaemuendesha Dubu.
Umbo lao lingine ni la Kijana Mzuri wa Kuvutia.
Umbo lao lingine ni la Mwanamke aliyebeba Kijiti cha
kukunjia Uzi chenye bonge la uzi.
Umbo lao lingine ni la Mbwa.
Umbo lao lingine ni la Dubu Jike.
Umbo lao lingine ni la Kunguru; Kunguru hawa hutumwa
kwenda kusaidia katika Kazi za Kichawi na Kijini kwa
Kuchukua Nguo za Ndani za Watu, Soksi, Vijiko, na vitu
vingine vidogo dogo kama hivyo. Ndio maana katika aina
nyingi za Ndege, Kunguru mara nyingi ndio huchukua
vitu vya ajabu ajabu ambavyo ndege wengine hawawezi
kuvichukua.
Umbo lao lingine ni la Nguo isiyo na mwili yenye
kubadilika badilika rangi.
Umbo lao lingine ni la Fimbo, Rungu, Bakora au Gongo
dogo.
hawa ndiyo majini wanaotawala siku ya jumatano
Majini wa jupiter(Mushtara) - Majini wa Alhamisi
Majini wa sayari hii wanakuwa na mwili mwekundu na
umbo la kati siyo wakubwa wala siyo wadogo, mwendo
wao na mwondoko wao ni wa kutisha na wa kuogopesha
lakini na wapole na wanao ongea taratibu.
Wana rangi ya chuma ambayo inawaunganisha wao na
Sayari ya Mars (Mariikh). Mwendo wao ni ule wa umeme
ukiambatana na ngurumo za radi.
Alama yao ni ya mizuka ya watu ambao miili yao ni kama
iliyojeruhiwa na Simba.
Umbo lao maalum ni la Mfalme mwenye Upanga akiwa
mgongoni mwa Simba akimwendesha.
Umbo lingine ni la Mtu aliyevalia rasmi Nguo za Chuma za
Kivita.
Umbo lingine ni la Kijakazi aliyevaa Taji lililopambwa kwa
Maua.
Umbo lingine ni la Ng’ombe Dume.
Umbo lingine ni la Paa dume
Umbo lingine ni la Tausi
Umbo lingine ni la Nguo ya rangi ya bluu isiyokua na
mwili.
Umbo lingine ni la Upanga.
Umbo lingine ni la Mti wa Mbuyu.
hawa ndiyo majini wanaotawala siku ya alhamisi
Majini wa Sayari ya Venus (Zuhura) - Majini wa Ijumaa
Majini wa Sayari ya Venus wana Umbo la kati na ambalo
ni zuri kwa kuliangalia ambapo sehemu yao ya juu ni ya
dhahabu na sehemu yao ya chini katika mwili ni ya rangi
nyeupe au kijani.
Mwendo wao ni kama wa mwendo wa Nyota inayong’aa.
Alama yao ni ile inayofanana na Wanawake wanaocheza
katikati ya Mduara, huku wakimshawishi na
kumtamanisha Mwanamazingaombwe ajiunge nao.
Umbo lao maalum ni ni la Mfalme aliyebeba Fimbo ya
Kifalme huku akiwa anamwendesha Ngamia.
Umbo lao lingine ni la Mwanamke aliye Uchi.
Umbo lao lingine ni la Mbuzi Mwanamke.
Umbo lao lingine ni la Ngamia; ambaye huwakilisha
Shetani mbaya aitwae Cazote.
Umbo lao lingine ni la Njiwa.
Umbo lao lingine ni la Nguo isiyokuwa na mwili ya rangi
Nyeupe au Kijani.
Umbo lao lingine ni la Mmea uitwao “Savine”.
hawa ndiyo majini wanaotawala siku ya ijumaa