Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 24 Aprili 2016

JINI AMLAWITI KIJANA KWA MIAKA 5 MFULULIZO!!!

Miongoni mwa mambo ambayo sitayasahau katika harakati zangu za tiba ni huyu kijana ambaye alikuwa akilawitiwa na shetani na huku shetani yule akijifanya ni jini mzuri kwa yule mtu wake bila yeye kujua.

Nakumbuka ilikuwa ni miaka2 iliyopita alikuja kijana na akatuelezea kuwa ana matatizo 2,la kwanza alidai kila inapofika usiku anakosa amani moyoni mwake kwani akipata tuu usingizi lazima aote analawitiwa na mwanaume mkubwa aliyevaa nguo nyeupe na mwenye misuli kama wacheza mieleka na akishtuka hujikuta na maumivu makali katika njia yake ya haja kubwa na hujihisi kuwa ameingiliwa kinyume na maumbile,hali hiyo ilizidi kuwa hivyo huku akiona aibu kueleza kwa watu lakini alipoona hali inazidi akaamua kuja kwetu kuomba msaada wa dua,na tatizo la pili ni kuwa na upungufu wa nguvu za kiume na hivyo uume wake kushindwa kabisa kutimiza majukumu yake

nilimuuliza historia yake ya siku za nyuma kidogo kabla hajaanza kuona hayo mambo yakimtokea akanieleza hivi''Mimi nilikuwa nafanya kazi ya ulinzi katika kampuni moja hapa hapa Dar,nilijitahidi kufanya kazi yangu kwa ufanisi mkubwa sababu nilikuwa naipenda sana hiyo kazi na nilipokuwa nikipata mshahara wangu mimi ni kulewa pombe,mzinifu na maasi mengine mengi,lakini ghafla nikajikuta sitamani kufanya ile kazi na siku moja nikajikuta kama nimechanganyikiwa(nilisimuliwa tuu maana sikuwa najielewa)kwamba niliwatukana viongozi wangu na wafanyakaz wenzangu kwa kuwa hawafanyi ibada,nilifanya vurugu nyingi na hatimaye nilitembea kwa miguu kutoka Dar mpk kwetu kibaha.Baada ya kufika nyumbani nilijiskia kuchoka sana nikapumzika bila kuongea na mtu na asubuhi ile hali ikanirudia tena nikaanza kuzunguka mitaani huku nikihubiri dini lkn bila kujitambua na hata kuwapiga sana wale ambao hawakuwa tayari kunisikilza,lakini baada ya kutokwa na hali hiyo nahuzunika sana  na kujishangaa mambo ninayoambiwa nimeyafanya na baada ya siku kadhaa ndiyo nikaanza kuota naingiliwa kinyume na maumbile mpaka leo.''

nikamuuliza ''hayo mambo unayoyahubiri uliwahi kusoma? akanijibu''hapana sijawahi kusoma kabisa kuhusu dini lakini huwa kuna wakati naskia sauti inanifundisha na vilevile nawaombea watu wanapona matatizo yao na ndiyo maana nikawa nashindwa kuomba ushauri kwao juu ya matatizo yangu mawili hayo.

mpaka hapo nikawa nimeshajua ni mchezo mchafu anachezewa na shetani tukaandaa sehemu ya kumfanyia dua alikaa kitako na kisomo kilianza.Kabla hatujafika mbali jini alipanda kichwani mwake na nikaanza kuzungumza nae kama ifuatavyo

Jini:assalaam aleykum 

mimi:wa alaykum salaam,wewe ni nani?

jini:mimi naitwa Malaikatu rruhaaniyya

mimi:Mbona Malaika hawamuhasi mwenyezi mungu wala kuwadhulumu wanadamu,sasa vipi malaika wewe mbona umehasi ni malaika wa wapi?

jini:mimi ni malaika niliyechanganyika na ibilisi

mimi:mmh ibilisi mbona hana uwezo wa kumpoteza malaika,iweje wewe uchanganyike na malaika mbona sikuelewi?

jini:kimyaaaa!!

mimi:hebu sema ukweli kabla sijachukua uamuzi wa kukufanya kitu kibaya maana unanipotezea muda!

jini:mimi ni jini sio malaika

mimi:lini umemuingia huyu jamaa?

jini:siku nyingi takribani inafika miaka mitano

mimi:umetumwa na mtu au ilikuwaje ukamuingia?

jini:hapana sijatumwa niliamua tuu,siku moja nilienda kazini kwao nikakuta wamefunga akanitolea maneno mabovu eti kwanini nimekuja muda ule kwani sijui utaratibu wa pale na alikuwa anaonekana amelewa,nilichukia sababu sipendi dharau,si angeniambia tuu kistaarabu.

mimi:jee unamuathiri kitu gani huyu mtu

jini:nimemvunja nguvu za kiume na kila siku namfanya mke wangu namlawiti mpaka niridhike!!!

mimi:kama unamfanya hivyo mbona pia anadai yeye anahubiri dini mitaani na kuwapiga watu wasiomuabudu mungu,inakuwaje hapa?

jini:akacheka kwa kebehi,huo ni ujanja wangu ili anione nina faida kwake na asinishitukie haraka

baada ya kupata maelezo hayo nikamuamrisha atoke kwa yule kijana na atubie dhambi zake asilimu na awe muislam

akanijibu
jini:mimi kwetu wote hawapendi hiyo dini nataka kusilimu lakini naogopa watanifunga jela au kuniua 

mimi:ukishasilimu usirudi tena kwao,utaelekea katikati ya majini wa kiislam wenzio nao watakulinda na kukupigania hawatokubali jini yeyote aje kukuchukua mbele yao.

akakubali akasilimu na akachagua jina Abdulkareem,nikamuelekeza wanakopatikana majini wa kiislam akaenda wakampokea na kuanza kumfundisha dini na maisha ya kumcha Mungu wa haki aliyeumba majini na binadamu kwa lengo la kumuabudu yakaanza.

basi yule kijana alikuwa ni kama mtu aliyetoka kwenye usingizi mzito,nikampatia baadhi ya dawa na tangu siku hiyo yale mambo yameisha na sasa ameoa na ana watoto wawili maisha yanaendelea.

MASHETANI WANA JANJA NYINGI SANA TUWE MAKINI!!!!!!!

muwe na siku njema!