Taratibu za utafutaji nyota zipo nyingi na katika mada ya leo nitazungumzia njia kadhaa.
wanadamu hatuna majina kwa sababu tuu wazazi wetu wametupatia majina hayo,bali majina yote yametoka kwa mwenyezi mungu kwani kwa mujibu wa vitabu vitkatifu vinaonyesha kuwa
1)kutajwa kuzaliwa kwa bwana yesu na jina lake halisi miaka mingi kabla ya kuzaliwa kwake
2) kuzaliwa kwa mtume Muhammad kwa jina hilo miaka elfu nyingi kabla ya kuzaliwa kwake
Hivyo tunapaswa kujua kwamba jina alilonalo mtu ndiyo jina hilohilo alilopewa na Muumba wetu na ndizo hulka alizomuumbia nazo kupitia kwa jina lake hilo.
NJIA YA KUTUMIA HERUFI YA MWANZO YA JINA LAKO NA TAREHE YA KUZALIWA
hapa chini kuna mpangilio wa nyota 12 kialfabeti,na pale alfabeti inapoangukia kwenye nambari fulani ndiyo nyota ya herufi hiyo na pia ndiyo nyota ya mtu muhusika ambaye ni herufi ya kwanza ya jina lake.na pia kama una yakini na tarehe yako ya kuzaliwa unaweza kutafuta kwa kuangalia tarehe hizo.
1.AMY= 1.PUNDA(ARIES)MARCH21-APRIL20
2.BNZ=2.NG'OMBE(TAURUS)APRIL21-MEI20
3.CO =3.MAPACHA(GEMINS)MEI21-JUNE20
4.DP = 4.KAA(CANCER)JUNE21-JULY20
5.EQ =5.SIMBA(LEO)JULY21-AUG21
6.FR = 6.MASHUK(VIRGO)AUG22-SEPT22
7.GS =7.MIZANI(LIBRA)SEPT23-OCT22
8.HT = 8.NGE(SCORPIO)OCT23-NOV22
9.IU =9.MISHALE(SAGITARIUS)NOV23-dec21
10.JV= 10.MBUZI(CAPRICON)DEC22-JAN19
11.KW =NDOO(AQUARIES)JAN20-FEB18
12.LX = SAMAKI(PIECES)FEB19-MARCH20
NJIA YA KUJUMLISHA HERUFI ZA MAJINA YAKO
ni vyema kutumia majina 3,jina lako,baba na mama
kabla ya yote kila herufi ni vizuri kama itapewa nambari yake kwa ajili ya kupata ukamilifu wa nyota ya mtu kwa kina zaidi .
jumlisha herufi zote za majina hayo na gawanya kwa jumla ya nyota 12itakayobaki hiyo ndiyo nyota ya mhusika
tazama mfano hapa chini
a=1,b=2,c=3,d=4,e=5,f=6,g=7,h=8,i=9,j=10,k=11,l=12,m=13,n=14,o=15,p=16,q=17,r=18,s=19,t=20,u=21,v=22,w=23,x=24 y=25,z=26
mfano
z u h u r a z a i n a s a l i m
26 21 8 21 18 1 26 1 9 14 1 19 1 12 9 13
jumla95 jumla51 jumla54
95+51+54
Zuhura Salim ambaye mama yake ni Zaina nyota yake ni NG'E
NJIA YA KUHESABU IDADI YA NAMBA ZA MAJINA 3 YA MTU
Katika njia hii ni kuhesabu tuu idadi ya namba za majina matatu ya mtu kama mfano uliotangulia na endapo idadi itazidi 12 unagawa kwa 12 baki ndiyo nyota ya muulizaji.lakini njia hii huwa inatoa taarifa kidogo sana ambayo inaweza kuathiri utimilifu wa nyota ya muulizaji.