Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Alhamisi, 14 Aprili 2016

MFAHAMU JINI CHEKETU JINI ANAYEPENDWA SANA NA WANGA


JINI CHEKETU NI NANI??
Huyu ni miongoni mwa mashetani hatari kabisa wanaotumiwa na kupendwa sana na wanga,jini huyu muhasi hutumiwa na wanga kwa kutumwa kwa mtu fulani ili amsababishie mambo yake yawe magumu,huwasaidia kuwapitisha wanga katika pembe za nyumba na kuingia ndani kuwanga,kila ukianzisha jambo linaishia njiani bila mafanikio,migogoro kwenye ndoa ni kazi ya jini huyu na pindi jini huyu akitumwa akuingie mwilini maisha yako yote utayaona magumu.
jini huyu akikuingia heshima yako itaporomoka,utadharaulika bila sababu,ataishusha nyota yako ya mafanikio hata ukiwa na elimu kila unachokifanya atakiharibu ili mradi uonekane hufai.
Pia ukiwa na jini huyu wewe utakuwa ni jumba la maradhi kwani ukiumwa ugonjwa huu ukijitibu mara unakuja ugonjwa mwingine,yaani ili mradi kila siku magonjwa tofauti tofauti
yote hayo jini huyu anaona hayatoshi ushenzi mkubwa zaidi anaoufanya ni pale wachawi wake wanapokwenda kwa mtu kumuwangia yeye huwageuza sura na kumuweka mmojawapo sura inayofanana na yako ili wale wanaowangiwa wakuone kama kwamba wewe ndiye mchawi  kumbe maskini huna hata unalolijua ila tuu ni mchezo wa jini huyu ili akutie ubayani.
Pia jini huy mshenzi hushirikiana na wanga katika kukupiga chale za wanga ambazo huwa ni kama alama zao popote uendapo

VIPI UTAJIJUA UMEINGIWA NA JINI CHEKETU?
Hizi ni baadhi ya dalili muhimu za mtu ambaye ameingiwa na jini wa cheketu

(1)kila uamkapo mwili unauma bila sababu
(2)kila unapokaa au kutembea unahisi unafuatwa na kivuli cha mtu
(3)Kila ufikapo usiku huwa unalala kupita kiasi
(4)Mwili kuchoka saana bila kufanya kazi yoyote
(5)kifua kubana
(6 )mbavu kuuma 

hapo juu nimekueleza kuwa pia jini huyu hushirikiana na wanga kukupiga chale mwilini mwako ambazo huwa kama alama kwao ngoja nikugusie kidogo .
aina za chale za wanga
1.chale za wanga wanaotaka kukufanya msukule
2.chale za kukukaribisha kwenye vikao vyao vya kichawi
3.chale za kukujulisha kwa wachawi kuwa wazazi/wazee wako wewe pia ni wachawi
4.chale za kuiba kivuli chako kitumike kwenye uchawi uonekane wewe mchawi
5.chale za mchawi mwenyewe zinamjulisha kwa wachawi wenzie kuwa ni mwenzao
wachawi wakikupiga chale zao kila chale ina maana yake waliyokusudia lakini kiujumla lazima
(1)Mambo yako kuwa magumu
(2)kujikuta umekatwa katwa mwilini wakati jana ulipoenda kulala ulikuwa safi
(2)kila ikifikaa saa 7mpaka 8usiku lazima ushituke
(3)utasingiziwa unawaroga watu mtaani kwenu
(4)utachukiwa na kuambiwa unaringa wakati kiuhalisia haupo hivyo 
ukiona hivyo jua kwamba wanga wamekupiga chale ambazo huwa kama muhuri popote uendapo utajulikana kwa chale hizo
                       
NJIA ZA KUFUTA CHALE ZA WANGA
( 1 ) Chukua kijiti cha wahenga
(2)Chukua fagio lilILotupwa
(3)Chukua sembe umeme
( 4) sembe mangube
(5)usila wa mti ulokufa wenyewe
(6)usila wa mti ulopigwa na radi
(7)sembe Makata
Mfute aliyepigwa chale kuanzia paji la uso 
hapo wanga hawatomuweza kumuona kwenye chombo chao

KUJIKINGA NA JINI HUYU WA KICHAWI
Soma sura hizi za kuran wakati unataka kulala hali ya kuwa pumzi yako inayotoka mdomoni inagonga kwenye viganja vyako vya mikono ulivyovikutanisha pamoja
Soma surat ikhlaasw x 7
soma Surat nnaas x7
soma surat lfalaq x7
soma surat fatha na usome ayaturkursiyyux 7 
kisha soma dua ya kulala na ujifute mwili wako wote kwa viganja hivyo kasoro sehemu za siri na chini ya nyayo za miguu.