Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumamosi, 17 Desemba 2016

MAHUSIANO YA NYOTA NA MAISHA YA MWANADAMU KWA MUJIBU WA QUR'AN


Katika elimu ya matibabu hutumiwa neno NYOTA kama nadharia ya kufikia lengo la kuponya maradhi ya mtu ya kimwili na kisaikolojia.

  Nyota ni lugha ya kidaktari ikimaanisha mafanikio ya Kiwango cha juu cha maisha ya mtu katika afya ya mwili na malengo ya kiuchumi.

  Nyota pia inawakilisha sayari zote zilizoangani na mizunguko (orbit) yake kwa mtu ili kufikia mafanikio hayo, na hapa ndipo linakuja suala la uhusiano wa nyota na mwili wa mtu.

Watu wengi hujiuliza maswali haya 
Je, ni kweli kuna uhusiano wa nyota angani na mtu?
Je, ni kweli kuna madhara au faida ya nyota angani kwa mtu?
Ukitaka kupata ukweli juu ya haya maswali ni vyema ukujua nadharia ya kidaktari katika elimu hii ya matibabu.

Moja ya nadharia za kitabibu ni "KUTAFAKARI TATIZO KABLA YA KULITATUA'
Hivyo basi ili upate kutoa tiba nzuri ni vyema kutafakari chanzo cha tatizo ndipo upate jinsi ya kutatua na matokeo yake.

DALILI JUU YA UHUSIANO WA SAYARI ANGANI NA MWANADAM
ALLAH anasema :
الله الذي خلق سبع سماوات ومن في الأرض مثلهن
Mwenyezi Mungu ni yule ambae ameziumba mbingu saba, na ardhi kuwa mfano wa hizo.
الطلاق :12
Q 65:12
Mfano wa sayari ya mwezi angani unavoathiri hapa duniani Inakuja kwa hadithi hii ya mtume (S. A. W) anasema :
كان رسول الله صلى الله عليه وسلم
قال إذا رأى الهلال
الله أكبر أللهم أهله علينا بالأمن والإيمان والسلامة والإسلام وتوفيق لما تحب وترضى ربنا وربك الله
رواه الترمذي :5/405
Mtume (s.a.w) aliyokuwa Akiona mwandamo wa mwezi mchanga anasema :
Mungu mkubwa, Ewe Mola wetu, kuchomoza kwa mwezi mchanga kwetu kuwe kwa Amani na Imani, na Salama na Uislam, na patanisho kwa yale anayoyapenda na kuyaridhia ALLAH, Mola wetu sisi na Mola wako wewe mwezi ni ALLAH (peke yake).
Hadithi hii yaonesha kuna madhara na faida kwa watu kwa kuandama kwa mwezi.
Mfano wa pili rejea Kitabu kinachoitwa
أسرار  العلاج بالحجامة والفصد
Ukurasa 44 - 45
Na hapa nanukuu machache tu zaidi usome mwenyewe
قد شرحه ابن سينا في
القانون حيث قال ويؤمر باستعمال الحجامة، لا في أول الشهر، لأن الاخلاط لا تكون قد تحركت وهاجت، ولا في أخره لأنها تكون قد نقصت، بل في وسط الشهر حين تكون الأخلاط هائجة بالغة في تزايدها لتزايد النور في جرم القمر..
يقول الدكتور ليبر
إن هناك علاقة قوية بين العدوان البشري والدورة القمرية
وهذه الحركة الكونية التي تتأثر بها الأرض، والأرض هي مكونة من ٧٠% و ٣٠% يابس هذه النسبة هي التي يتكون منها جسم الإنسان
Ibn Sina anasema :jambo la Hijama halifanywi mwanzo wa mwezi wala mwisho wa mwezi bali ni bora liwe katikati ya mwezi kwa kuwa wakati huo ni mzuri kwa jambo hilo.
Na Dr mwingine anasema ;hakika hapa kuna nguvu ya mvutano baina ya mwili wa mwanadamu na mizunguko wa mwezi.
Huu mzunguko ni wa kawaida ambao huathiri ardhini, kwa kawaida ardhi ina 70% ya maji na 30% ya nchi kavu na viwango hivi vinasabishwa na mwili wa mwanadamu ambao 70% ni damu na 30% ni viungo vingine. Maji ni sawa na damu hivo maji yakitulia na damu hutulia.
Katikati ya mwezi maji ya bahari hutulia na damu hutulia mwilini na huo ni wakati mzuri kutibia kwa njia ya Hijama.
Kwa maelekezo hayo inatosha kujua kuwa upo uhusiano mkubwa wa sayari zetu na maumbile ya mwanadamu.