Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 11 Septemba 2017

Faida ya mbegu za maboga kiafya na kitiba.




Ulaji wa mbegu za maboga una faida nyingi kwenye mwili wa binadamu lakin ni waTanzania wachache sana wanaofahamu umuhimu huo.
Mbegu za maboga zina kazi lukuki kiafya ktk mwili pia ni tiba ya magonjwa makubwa sana kutokani na wingi wa madini uliopo kwenye mbegu hizo kama chuma,zink,manganese,na kopa.
Mbegu za maboga huweza kuliwa kwa kutafuna baada ya kuanikwa juani,au zikiwa zimekaangwa kwenye sufuria kwa moto hafifu au unga wake kuchanganya ktk maziwa au uji.
magonjwa yanayotibiwa ama kukingwa kwa ulaji wa mbegu za maboga.

1.kibofu cha mkojo.Mbegu hizi hutibu kibofu cha mkojo na imetumika kwa muda mrefu sana ktk swala hili has a kwa wanaume.
2. Kinga ya mwili.Kutokana na wingi wa madini ya zinc mbegu hizi husaidia kinga ya mwili ,husaidia ukuaji na kuondoa homa za Mara kwa Mara. Pia huleta usingizi kwa wenye tatizo la kukosa usingizi pia hufanya mwili kutochokachoka .
3.nguvu za kiume.Habari iliyothibitika mbegu hizi ni zaidi ya supu ya pweza kwenye swala hili.
Mbegu hizi huongeza nguvu pamoja na manii kwa mlaji.pia hutibu nguvu hata kama mlaji ana sukari nyingi kwa sababu mbegu hizi hushusha na kusawazisha kiwango cha sukari mwilini halaka sana.
5. Hutibu moyo.Watu wenye matatizo ya moyo ,presha zote mbili mbegu hizi ni tiba kubwa sana ya kutibu,kuimarisha na kusafisha moyo pamoja na mishipa yake.
6.afya kwa Mtoto mchanga na mama mjamzito.
Kama chakula cha Mtoto kitasagwa pamoja na mbegu hizi basi Mtoto hataumwaumwa,atakuwa na afya,nguvu na kunawili. Pia husaidia Mtoto kupata usingizi .kutokana na kirutubisho cha omega 3 fat basi mbegu hizi
Huzuia pia mama mjamzito kuzaa Mtoto njiti ama asiye na afya.
7. Kinga ya saratani.
Mbegu hizi hukinga saratani zote mwilini.
8. INI na moyo.Ulaji wa mbegu hizi hutibu magonjwa ya moyo na INI na kuimarisha afya ya viungo hivyo muhimu sana.
9. Hutibu kisukari.
Kwa Mwenye kisukari akila kila siku mbegu hizi basi sukari itakaa vizuri na itashuka.
Tiba ya usingizi.
Kwa wanaokosa usingizi wajitahidi kula mbegu hizi.
11. Hupunguza KITAMBI na uzito.
Ulaji wa mbegu hizi ndani ya miezi mitatu itakuwezesha kupunguza kilo 20 hadi 30 pia hupunguza KITAMBI kwa njia salama na ya afya.
Matumizi.Hakikisha unatafuna robo kikombe cha chai kila siku.
Waweza kuzikanga kwa moto hafifu japo kufanya hivyo huonda mafuta ambayo ni muhimu sana kwa afya yako.
Pia waweza nunua ya unga ukawa unaweka kwenye maziwa ,uji ama maji ya moto kama huna muda wa kutafuna.