Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Alhamisi, 19 Aprili 2018

vifuatavyo ndyo vyakula wanavyotakiwa kula wagonjwa wa sukari



wagonjwa wa sukari mmekuwa mnanipigia simu na kuniuliza sana kuhusu hili,leo nimeamua kuwawekea hapa kila mtu anufaike

Wagonjwa wa kisukari wanashauriwa kula vyakula vifuatavyo.
KACHUMBARI.
Kachumbari ina viungu vya mimea ambavyo vyote hupunguza kiasi cha sukari mwilini. Kachumbari hiyo inalazimika itengenezwe na nyanya, vitunguu, karoti na tangawizi.
Tibazetu.blogspot.com
Ulaji wa kachumbari inatakiwa iliwe kila baada ya masaa nane. Kwa hiyo upatapo breakfast yako asubuhi anapaswa upewe na kachumbari.
MBOGA ZA MAJANI
Mboga za majani zinazoongoza kushusha kisukari ni spinachi, mgagani, matembele na bamia.
VYAKULA VYA WANGA.
Pamoja na ukweli kwamba kisukari kimesababishwa kwa kula vyakula vya wanga kupita kiasi lakini vipo vyakula vya wanga ambavyo hushusha sukari mwilini kama vile viazi vitamu, ndizi mbivu na pia kuna chakula cha kienyeji maarufu kwa mikoa ya kusini kiitwacho kikandi.
Tibazetu.blogspot.com
VYAKULA VYA PROTEINS
Mgonjwa wa kisukari anaruhusiwa kula aina zote za proteins kama vile nyama, samaki, ndege, wadudu na mayai. Lakini proteins hizo hazitakiwi ziambatane na mafuta yake. Kama ni nyama, samaki na ndege( kuku) itapaswa ichomwe kwanza kwa lengo la kuondoa mafuta kisha iandaliwe atakavyopenda mgonjwa.
MAFUTA.
Licha ya ukweli kuwa mafuta yanachangia homa ya kisukari lakini imegundulika mafuta ya nazi na ya mzeituni hupunguza kiasi kikubwa cha kisukari mwilini.
VINYWAJI
Tibazetu.blogspot.com
Mgonjwa wa kisukari anashauriwa kunywa chai ya majani ya mlonge au mwarobaini au leonotis leonurus au ocimum gratessimum( manunga nunga)
Pia anashauriwa kunywa juice ya mpapai, alvocado, mpera, embe na nanasi.
POMBE NI MARUFUKU.
Mgonjwa wa kisukari ni marufuku kunywa pombe kwa hoja kuwa kiwango cha sukari na wanga kilichopo kwenye pombe kitazidisha maradufu sukari mwilini.
Kwa tiba za asili juu ya magonjwa sugu mbalimbali wasiliana nasi
+255 657739713
+255 764995259
Tibazetutz@gmail