Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatano, 4 Januari 2017

Anaswa na polisi akifukua kaburi la albino

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kufukua kaburi la marehemu ambaye likuwa ni mlemavu wa ngozi (Albino) aliyefariki mwaka 2010 kwa lengo la kuchukua viungo vyake.

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na Kamanda a Polisi Mkoani Mbeya DCP Dhahiri Kidavashari inasema kuwa mnamo tarehe 03.01.2017 majira ya saa 01:00 usiku katika Kijiji cha Mumba kilichopo Kata ya Ilembo, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JONAS JOHN mkazi wa Chapakazi alikamatwa na askari Polisi akiwa na wenzake wawili wakifukua kaburi la marehemu SISTER OSISARA aliyekuwa mlemavu wa ngozi (ALBINO)

Inadaiwa kuwa marehemu alifariki dunia mwaka 2010 kwa ugonjwa wa homa na kuzikwa katika makaburi ya Kijiji cha Mumba.

Mtuhumiwa alikutwa na majembe na makoleo ambayo walikuwa wakiyatumia kufukuria kaburi hilo. Baada ya mahojiano mtuhumwa huyo aliwataja washirika wenzake wawili ambao walikimbia baada ya kuwaona askari.

Jeshi hilo linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa .