Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatano, 18 Januari 2017

TUMUANGALIE JINI BURHANI,JINI MTOA TAARIFA KWA KITI WAKE


* Jini huyu ni jini aina ya ruhani, ni jini mzuri sana

* Huyu ndio jini anaefanya kazi ya kukusanya 
taarifa mbalimbali na kumpelekea mhusika
wa jini huyu.

*Buruani ni bingwa wa kuona, kuangalizia na
kufahamu majambo mbalimbali hapa
duniani.

*Ukiwa nae huyu jini usitemegee kwamba ipo
siku atapanda na kuzungumza hapana si kazi
yake kupanda na kuzungumza.
*Ila atakuja kwako kwa nyingine ili akufahamishe
mfano katika ndoto na n.K.


DALILI ZA BURUHANI
* Kuna wakati unaweza ukajikuta upo kwenye sehem ya hatari lakini ghafra ukajikuta akili yako inakutuma usifanye hilo jambo ama  usipite hiyo njia ama ukaamua kukaa kimya kwa muda.Yani bila ya hata wewe kutambua na ukajikuta umeepuka matatizo mengi sana.
HUYO NDIO BURUHANI.

*Kuna wakati ukajikuta wewe unakuwa mtu wa 

kuhisi jambo na likawa hivyo hivyo mfano ukaisi kesho mvua itanyesha na ikanyesha kweli na unaweza ukakaa sehemu lakini ukajikuta kama kuna mtu anakunogeneza masikioni unyanyuke na uondoke hapo ulipo na kama ukiondoka utajikuta umeiepuka shari 

* Unaweza ukajikuta unamwambia mtu ya 
kwamba anaweza akakutwa na tatizo huko anapokwenda na kweli akienda linampata la kumpata.HUYO NDIO BURUHANI.

*Unaweza ukalala na ukajikuta unaota ndoto ya 
jambo fulani litakutokea na baada ya siku kaadha likakutokea kama ulivyoota,halafu ukawa unajishangaa mbona nikiota jambo
lazima litatokea kweli.

* Unajikuta unaota msiba wa flani na baada ya 
muda msiba ukawepo. Yaani taarifa zote za kitabibu kwa watu wa tiba huyu jini ndo anazikusanya na kuziwasilisha kwa majini wenzake ndipo hatua zingine zinafuata

ANAFANYAJE KAZI ZAKE KWA MGANGA WA MARUANI.
* Unaweza ukamkuta mganga anakupigia ramli kwa kutumia jini maimuna, makatani, beduani
n.k lakini kazi ya uchunguzi, ugunduzi na uangalizi anapelekewa BURUHANI na akitambua tatizo ni nini anawasilisha kwa jini mpiga ramli tatizo lako ili lifanyiwe kazi.

*Kwaiyo swala la uchunguzi wa BURUHANI 
nikimaanisha uwezo wa kuchunguza na 
kufahamu majambo inategemea baina ya BURUHANI na BURUHANI kuna wengine wana elimu kubwa ya uchunguzi lakini wengine elimu yao ndogo kutegemea na mazingira ya
jini n.k