Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumamosi, 14 Januari 2017

FUNGA NDOA KIURAHISI KUPITIA NYOTA


NYOTA YA PUNDA NA MIZANI
Mpate mpenzi siku ya Ijumaa kwenye sherehe za ngoma saa 3 au saa 9, vaa nguo rangi mbili juu nyekundu chini njano.
Mshike mkono mara kwa mara, hakikisha mnakula kabla ya mazungumzo

NYOTA YA NGOMBE NA NGE
Ng’ombe: kutana nae saa nane na uwe peke yako, Vaa nguo ya rangi ya kijani iwe siku ya Jumanne saa 2 au saa 8.
Mpe chakula cha mafuta mafuta na rojo rojo. Mkutanishe na jamaa zako wa nyumbani usimtazame usoni, mguse guse shingo na mapaja.
Penda kuimba imba au vaa Walkman.
Tendo la ndoa liwe refu na la kurudia rudia.

NYOTA YA MAPACHA NA MSHALE
Penda sana kuzungumza kiingereza au kusoma soma na kushika gazeti unapotembea mbele yake.
Kutana nae siku ya Jumatano saa 9 na mpende ndugu yake wa pili.
Penda kutafuna tafuna Big G na zungumza utani kwa wingi huku ukizungumza upesi upesi.
Vaa nguo za kitoto fupi na usikose mkanda.

NYOTA YA KAA NA MBUZI
Penda sana kununa, usicheke hovyo, mpe vitu baridi kama peremende, ice cream, na vitu vya kunyonya.
Mvamie na umshike shike kitovu pia mfinye finye vidole.
Tembea nae taratibu na uzungumze nae pole pole, penda sana mambo yake.
Vaa nguo ya rangi ya bluu isiyoiva. Lazima muishi sehemu za bondeni na nyumba yenu iwe na choo cha ndani na sehemu ya kulia chakula.
Kutana nae Jumamosi au Jumapili saa 4 au saa 10.
Zungumza nae kwa kigugumizi.

NYOTA YA SIMBA NA NDOO
Mpenzi anapenda kukandwa na hapendi kutolewa ukali na mtembea kwa haraka, saa za mapumziko ziwe saa 1 na saa 5.
Uwe muhongaji na ukae karibu na nyumba ya kona. Mwanamke avae Kofia au Ushungi na kiuno akibane kwa Mshipi au kanga.
Tendo la ndoa liwe fupi na la kurudia lakini pendelea kukandana.
Kutana nae siku ya Jumapili ambayo ndio siku ya Mapenzi.

NYOTA YA MASHUKE NA SAMAKI
Chagua mpenzi asiesoma zaidi kuliko aliyesoma, utampata mpenzi wa ndoa mnamo tarehe 30 na huenda mkakutana hospitali au hotelini au baada ya ajali.
Kuwa maridadi, vaa viatu virefu vya kisigino na mlio. Usikose senti kidogo na usioneshe kulia au kukata tamaa na kumuhudumia katika ugonjwa wake au jamaa wake wa kike. Kutaneni siku ya Alhamisi.