Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 31 Januari 2017

MAWASILIANO YA KIROHO HUDUMU DAIMA!

Wanasayansi wanaita elimu za kufikirika eti kwakuwa tu hazina ithibati za kisayansi...! Wanashindwa kutambua jambo moja muhimu sana kwamba hata ithibati hizo za kisayansi chanzo chake ni roho na ufahamu..kwahiyo bila rohohai bila ufahamu hakuna sayansi wala ithibati zake.

Ndoa za kikristo zina kiapo kisemacho ...'nitakuwa pamoja nawe katika hali ya dhiki na katika hali ya uzima...hadi KIFO KITAKAPOTUTENGANISHA...!!! Kiapo muhimu sana hiki.

Bahati mbaya haikufafanuliwa kuwa kifo kitatutenganishaje! Tafsiri yake hapa ni kwamba hadi kifo kitakapotutenganisha kimwili....!!! Kiroho mawasiliano yako pale pale kila siku kila saa kila dakika.
Roho ikisha zaliwa haifi huishi milele, kinachokufa ni mwili huu uharibikao
Tuna shuhuda nyingi tu hata hapa jukwaani la watu kutokewa ndotoni na wapendwa ndugu na hata jamaa waliokwisha tangulia kifoni.

Kwa hali ya kawaida ya kibinadamu tunaita ni ndoto lakini kwenye ulimwengu wa roho si ndoto bali ni mawasiliano ya kiroho kati ya watu wawili wanaofahamiana vema na Kwa baadhi ya matukio wasiofahamiana kivile

Kulala usingizi ni sawa na kuwa nusu mfu..unapumua lakini huna fahamu na hujui kinachoendelea...hiki ndio kipindi ambacho mawasiliano ya kiroho huchukua hatamu na kufanya kazi yake barabara huku ufahamu ndani ya mwili uharibikao ukiwa umepumzishwa.

Hali zote hizo hutokea usingizini na ikitokea marehemu amekutokea live ukiwa na fahamu zako kamili huyo hajafa bali kapotezwa kimiujiza huku mkiaminishwa kuwa alikufa na mkamzika na matanga mkakaa

Tunaishi kwenye dunia ya elimu finyu inayotunyima uhuru na uwazi wa kuyafahamu mengi, elimu yetu ni ya njia moja kusoma ili upate kazi itakayokuletea kipato baaassi....!!!

Lakini tuna mengi hatujayafahamu hatujafunuliwa hatujayatafakari na kuwa na uwezo wa kuyahoji na kuyajengea mijadala

Najua wengi tutaota usiku huu...! Ndoto ni hitaji la kiasili la mwanadamu na kati ya ndoto tutakazoota leo tukiwa usingizini fofofo ni ndoto zinazohusika na wale waliotutangulia kifoni....! Tafakari kila ndoto Kwa ukamilifu wake kwakuwa sehemu kubwa ya ndoto ni mawasiliano ya kiroho