Ni mboga maarufu miongoni mwa Watanzania. Mbali na kutumiwa kama mboga, mchicha pia ni tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mchicha unaweza kutibu matatizo yafuatayo :
Kuumwa mgongo
Kusafisha njia ya mkojo
Kusafisha damu
Unatibu Magonjwa ya Figo
Unatibu minyoo
Unatibu Baridi yabisi
Tezi la shingo
Homa
Kuongeza damu
Unasaidia kupata haja ndogo kwa wingi
Unarutubisha uwezo wa kuona vizuri.
JINSI YA KUTUMIA MCHICHA KAMA DAWA
MATAYARISHO
Chukua mchicha kilo 1 ya mchicha, chemsha maji lita 2 na nusu. Yakichemka loweka mchicha kwa dakika 15. Tumia kikombe. Ni bora utumie yote kwa siku . Dozi ni siku 5
KAMA UNATAKA KUTIBU MGONGO:
Chukua mchicha ponda. Chua mara 3 kwa siku. Usiku unapasha moto mchicha kisha unufunga mahali panapouma. Lala nao wakati vuguvugu la joto lake lenye maji ndani (dawa) ikiingia ndani fanya hivyo kwa siku 5, ukibadilisha kila siku (fresh)
KUTUMIA MCHICHA KAMA TIBA YA TEZI LA SHINGO
Chukua mchicha kiasi kidogo, ponda, fungia shingoni pale penye uvimbe wakati unapolala kwa kitambaa, kwa muda wa siku 5.
Mwenyezi Mungu anatibu
Sisi ni sababu